Na Jumia Travel Tanzania
Kama umeshawahi kusafiri kwa ndege
naamini utakuwa unafahamu ni kitu gani cha kubeba kwenye begi lako na
kipi sio. Endapo haujawahi au unatarajia kufanya hivyo kwa siku za hivi
karibuni basi usafiri huo una masharti na taratibu zake ambazo ni lazima
zifuatwe vinginevyo hautoweza kuutumia.
Tofauti
na usafiri wa kawaida kama vile mabasi ambayo watanzania wengi
tunayatumia ambapo ni mara chache kukuta kunakuwa na upekuzi mkali wa
abiria mbali na tiketi zao, Jumia Travel ingependa kukufahamisha kwamba
kusafiri kwa kutumia ndege kuna masharti na taratibu ambazo kila abiria
ni lazima azifuate na kuzizingatia ndipo aruhusiwe kuingia ndani.
Vifaa vyenye ncha kali.
Hairuhusiwi kabisa kubeba vitu vyenye ncha kali kama vile kisu, wembe,
mkasi, bisibisi au panga kwenye begi lako la kusafiria labda iwe kwenye
mzigo tofauti ambao utapekuliwa na kupewa kibali. Kwa ufupi kama
unadhani utahitajika kuvibeba ni vema kuviweka kwenye mzigo tofauti ili
vifanyiwe upekuzi ndipo uruhusiwe. Tofauti na hapo ili kuepuka usumbufu
au kuchelewa safari yako basi unashauriwa kuwasiliana mapema na shirika
la ndege utakalosafiri nalo kwa msaada zaidi.
Silaha za moto.
Hakuna silaha inayoruhusiwa kubebwa kwenye begi lako la kusafiria kwa
sababu za usalama wako na abiria wengine kwenye ndege. Ingawa taratibu
hutofautiana baina ya nchi au mashirika ya ndege lakini asilimia kubwa
vitu hivyo huwa haviruhisiwi kabisa labda kuwa na sababu na kibali
maalumu.
Vitu vinavyoweza kulipuka.
Kuna baadhi ya bidhaa tunazitumia ambazo ndani yake zina kemikali
ambazo hulipuka kwa urahisi bila ya kujua. Kwa mfano, takribani marashi
yote ya kujipulizia mwilini (body spray) au vibiriti vya gesi huwa na
kemikali ambazo zinaweza kulipuka kwa urahisi na ndiyo maana huwekwa
alama ya moto (inflamable). Hivyo basi ni vema kulijua hilo ili
unaposafiri usibebe maana utaishia kwenda kuyaacha mahala pa ukaguzi
kabla ya kupanda ndege.
Vifaa vya michezo.
Kuna baadhi ya vifaa vya michezo vinachukuliwa kama silaha. Kwa mfano,
vifaa vya kuchezea gofu, tenesi, mpira wa magongo, upinde na mkuki na
kadhalika. Kwa mfano, timu nyingi za michezo mbalimbali zinaposafiri
vifaa hivi huwekwa kwenye mizigo tofauti na ile ya wachezaji kwa ajili
ya ukaguzi ili kuepusha usumbufu.
Vifaa vya kazi.
Inawezekana ukawa ni fundi mzuri na una wateja takribani kila kona ya
nchi hivyo ukahitajika kusafiri kwenda kufanya kazi. Itakuwa ni jambo la
busara ukafahamu mapema kwamba kusafiri kwenye begi lako na vifaa vyako
vya kazi kama vile nyundo, msumeno, patasi au bisibisi itakuwa ngumu.
Utaweza kufanya hivyo pale tu utakapovifungasha kwenye mzigo wake
tofauti ili ukaguliwe kwa ajili ya usalama wako.
Dawa za binadamu. Kuna
wakati unaweza ukawa na matatizo ya kiafya lakini ukahitajika kusafiri
hivyo ni vema kujua pia kuna taratibu za kusafiri na dawa zako za
matibabu. Iwe unasafiri ndani au nje ya nchi vitu muhimu vya kuzingatia
ni pamoja na barua au maelezo ya daktari kuhusu ugonjwa wako pamoja na
dawa alizopendekeza kuzitumia na kubeba. Kwa hiyo ili kuepuka kuzuiwa
kusafiri na dawa wakati mwingine itakuwa vizuri hata ukawasiliana na
shirika la ndege utalosafiri nalo ili ujue taratibu zao zikoje.
Vimiminika.
Unaweza ukashangaa kwanini hautoruhusiwa kusafiri na maji yako ya
kunywa ambayo umeyabeba kwenye begi lako. Ingawa sheria hutofautiana kwa
baadhi ya nchi ambazo huruhusu kiwango fulani kwa hapa Tanzania hali ni
tofauti. kwenye kundi hili maziwa ya chupa na madawa hayaingii kwenye
kundi hili ingawa ni lazima yaambatinishwe na maelezo au kibali maalum.
Bangi. Nadhani
hili linaeleweka miongoni mwa watu wengi kwamba Tanzania kilevi hicho
ni marufuku kukitumia kwa hiyo kukutwa nacho tu ni uvunjaji wa sheria.
Kuna baadhi ya nchi zinaruhusu aina ya kilevi hicho kana kwamba mpaka
madaktari hutoa vibali kabisa kwa wagonjwa wao kutumia. Ila kwa nchi ya
Tanzania bangi ni marufuku na ukikutwa nayo utachukuliwa hatua za
kisheria.
Kwa
kawaida mtu wa kawaida anaposafiri kwa kutumia ndege kunakuwa hakuna
vitu vingi vya kuhofia kwani ni mara chache vitu hivyo huhitajika
kubebwa. Mbali na hapo utajitafutia matatizo au kuhatarisha usalama wa
abiria wenzako. Jumia Travel
imeona ni vema kukutahadhirisha kwamba kutokana na kuongezeka kwa
matukio ya kutishia usalama kupitia usafiri huo, hatua kali zimekuwa
zikichukuliwa na nchi mbalimbali duniani.
SHARE
No comments:
Post a Comment