Afisa Matukio wa Airtel Tanzania akikabidhi simu maalum
zitakazotumika kuendesha mradi wa VSOMO kwa Msajili
Mkuu Veta Kipawa(Registry), Bw, Harold Mganga, (kushoto), akishuhudiwa na Mratibu wa Miradi na Kozi fupi.
(Project and Short Course Coordinator)Veta Kipawa Gosbert Kakiziba (katikati)
simu hizo zimetolewa kwa kwaajili ya mradi wa VSOMO. VSOMO ni
applikesheni maalum inayotoa mafunzo ya ufundi stadi ya VETA kwa njia ya
mtandao inayodhaminiwa na Airtel Tanzania.
Afisa Matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kulia) akimuonesha
applikesheni ya VSOMO Mkuu
wa Usajili Veta Kipawa, Harold Mganga (katikati) pamoja na Mratibu wa Miradi na Kozi fupi.
(Project and Short Course Coordinator) Veta Kipawa, Gosbert Kakiziba (kulia). hafla
fupi ya makabidhiano ya simu hizo yaliyofanyika Veta Kipawa. Aplikesheni
ya VSOMO inatoa mafunzo ya ufundi stadi ya VETA kwa njia ya mtandao
inayodhaminiwa na Airtel Tanzania.
Mamlaka
ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) kwa kupitia mfumo wa mafunzo kwa
mtandao wa VSOMO unaodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
imebainisha kuwa iko tayari kuhudumia vikundi au jamii ya wanaotaka
kujifunza ufundi stadi kwa kupeleka timu yao ya mafunzo kwa vitendo
popote ili kuhakikisha dhana ya uchumi wa viwanda inakamilika kwa kuwa
na mafundi wazuri waliohitimu ufundi katika chuo maalumu nchini
Hayo yamebainishwa na mkuu wa chuo cha veta kipawa ambae pia ni msimamizi wa mradi wa mafunzo kwa njia ya simu unaodhaminiwa a Airtel kwa lengo la kutoa FURSA kwa vijana wegi mjini kupata ujuzi na kujiajiri Mhandisi Lucius Luteganya.
VETA tuko tayari kuwafuata wanafunzi wetu endapo watajiandikisha na kuhamasihana kwa kikundi kusoma kwa njia ya mtandao wa VSOMO , ikiwa watakuwa vijana kuanzia 15-20 na wakipenda kupata mafunzo waliko basi sisi tutawafuata waliko ili kuhakikisha wanahudumiwa na mobile trainers wetu”
“sasa hivi kupitia mtandao wa Vsomo tunakozi 12, wanafunzi wanaweza wakajisomea wawapo popote mara baada ya kupakua App yetu ya VSOMO na kulipia kozi anayotaka” alisisitiza Luteganya.
Luteganja alitaja kozi hizo kuwa ni “Tunampango waongeza kozi zingine
15 hivi karibuni lakini kwa sasa zilizopo tayari kwenye mtandao ni
Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta,
umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani , Umeme wa magari, Ufundi
umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi
Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea
vyuma.
Tangu VETA na Airtel walipozindua mfumo huu wa mafunzo kwa njia ya mtandao waVSOMO mwezi wa Juni 2016 Mfumo huu wa VSOMO sasani umepata umaarufu mkubwa kwa vijana ambapo takwimu zinaonyesha zaidi ya vijana 30,000 tayari wamepakua application ya VSOMO, 8000 wamejiandikisha na kati yao 50 wameshasoma kozi mbalimbali na kupata vyeti vyao vya ufundi stadi kutoka VETA.
Kujiandikisha katika mojawapo ya kozi 12 zinazopatikana katika application ya VSOMO mwanafunzi atalipia kwa simu yake gharama ndogo ya shilingi 120,000 tu kupitia huduma ya Airtel Money kwa kupiga *150*60#. na kufanya malipo ambazo gharama hizi zitamuwezesha kuja kupata mafunzo kwa vitendo bila malipo ya ziada.
SHARE
No comments:
Post a Comment