Meneja
Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) akiongea wakati wa
kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama yatakayotolewa katika maabara
iliyopo katika shule ya msingi ya Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati
ya Airtel Tanzania na Atimizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi).
Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa DTBi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Mhandisi George
Mulamula (kushoto) akiongea wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya
Tehama yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya
Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya
Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi). Kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel
Tanzania Jackson Mmbando.
Mwanafunzi
wa darasa la nne wa shule ya Msingi ya Kijitonyama Mariam Said
akionyesha ujuzi wa kutumia kompyuta huku akishuhudiwa na Mkurugenzi
Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Mhandisi George
Mulamula (kushoto) na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando
(kulia) wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama
yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya
Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya
Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi).
Mwanafunzi
wa darasa la nne wa shule ya Msingi ya Kijitonyama Karim Ramadhan
akionyesha ujuzi wa kutumia kompyuta huku akishuhudiwa na Mkurugenzi
Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Mhandisi George
Mulamula (kushoto) na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando
(kulia) wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama
yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya
Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya
Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi).
Airtel
kwa kushirikian na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) leo
imetangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehema yatakayotolewa katika maabara
iliyopo katika shule ya msingi Kijitonyama na kuwaalika wanafunzi wa
shule za msingi, sekondari, wanavyuo na jamii yote kwa ujumla
kujiandikisha katika mafunzo yatakayowapatia ujuzi utakaochochea
kuondoa umasikini na kukuza technolojia.
Maabara
ilianzia kama kituo cha kutoa elimu ya Tehama mwezi Julai 2017 kwa
lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi katika masomo ya Tehama
yatakayosaidia matumizi ya teknolojia na Tehama katika biashara.
Maabara hii kwa sasa itaanza kufanya kazi kwa kutoa masomo mbalimbali
ambayo ni pamoja na lego Robotics, program za uhuishaji kwa
watoto(ziitwazo scratch) na ubunifu na uchapishaji wa“3D objects”
pamoja na msingi wa kompyuta, uelewa wa kompyuta, kutengeneza program
mbali mbali ,mtandaousalama wa mtandao
Akitangaza
program hizo, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania , Jackson Mmbando alisema
“ Tumeanzisha maabara hii ya kompyuta kwa lengo la kuwawezesha
wanafunzi na waalimu wa shule ya msingi pamoja na vijana wanaopenda
kujikita kwenye masomo ya sayansi na Tehama kupata ujuzi wakiwa katika
umri mdogo. Lengo letu ni kuendelea kuiwezesha sekta ya technolojia na
Tehama kukua na kuzalisha vijana ambao wataweza kuvumbua na kutengeneza
programu zitakazoleta suluhuhisho kwenye mahitaji ya biashara naustawi
wa jamii. Tunaamini maabara hii ni jukwaa la kukuza vipaji vya vijana
na Airtel inajisikia fahari kuwa sehemu ya kuleta mapinduzi na
mabadiliko haya katika jamii na nchi kwa ujumla ikiwa ni mwendelezo wa
program ya Airtel Fursa inayoendeshwa na Airtel”.
Mmbando
alieleza kuwa maabara hii itatoa mfunzo bure kwa walimu na wanafunzi wa
shule ya msingi Kijitonyama ila kwa kijana yeyote asiyekua mwanafunzi
au mwalimu wa shule hii atakayependa kujiandikisha ataruhusiwa kufanya
hivyo.
Fomu
za kujiandikisha zitapatikana kwa njia ya mtandao kwa gharama ya
shilingi 20,000 kupitia www.teknohama.or.tz na www.airtelfursa.com au
kwa kutembelea maabara iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama
kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 mchana. Mafunzo yatatolewa kwa wiki 4
kuanzia tarehe 4 septemba 2017.
“natoa
wito kwa vijana hususani wanafunzi wa shule ya msingi kijitonyama na
maeneo ya jirani kutumia fursa hii kujiendeleza zaidi”. Aliongeza
Mmbando.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Mhandisi George Mulamula alisema “ pamoja na kuwa na wahitimu kutoka katika vyuo mbalimbali lakini bado Tanzania tuna uhaba wa wataalamu wabunifu wenye ujuzi wa kutengeneza program u zitakazotatua changamoto za kijamii za kibiashara na zinazokuza kipato na kuondoa umasikini”
“Maabara
hii ina malengo mawili: kuwatayarisha vijana wanaotarajiwa kwenda chuo
kikuu kuwa na elimu ya kibiashara ya Tehama zaidi ya kuwa na uelewa wa
kompyuta na programu za simu. Lakini pili kuwaunganisha na wadau wa
kibiashara ili kuwapa mwelekeo utakaowawezesha kutoa suluhisho la
kiteknolojia na Tehama zitakazosaidia nchi kufikia malengo yake ya 2015
ya uchumi wa viwanda pindi watakapohitimu shule.
DTBi inaishukuru sana Airtel na uongozi wa shule ya Msingi Kijitonyama kwa kuungana nasi na kuwa sehemu ya kuleta mapinduzi haya ya Tehama kwa jamii na katika biashara kwa ujumla” alisema Mulamula
Aliongeza
kwa kusema huu ni mwanzo tu kwani walimu, vijana na jamiii watapata
ujuzi na ni matumaini yetu programu hii pia itafika maeneo mbalimbali
nchini.
DTBi
kama msimamizi wa masomo wana timu ya wataalamu ambao wamejitolea kutoa
mafunzo kwa vijana na kuleta mabadiliko katika jamii. Tunawakaribisha
wale watakaopenda kushirikiana nasi kujiunga sasa, alimalizia.
SHARE
No comments:
Post a Comment