
Mhashamu Askofu wa Kanisa
Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiongoza Ibada ya
Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John
Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya
Mtakatifu John Mjini Bariadi katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara
iliyoongozwa na Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA
Liberatus Sangu.

Mhashamu Askofu wa Kanisa
Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiwapaka mafuta vijana wa
Kipaimara katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika
Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.

Mhashamu Askofu wa Kanisa
Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiwabariki vijana wa
Kipaimara katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika
Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.

Baadhi ya Vijana waliopata
Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John
Mjini Bariadi wakiimba katika ibada .

Kwaya ya Shirikisho ikiimba
katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa
Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.

Ndg. Vincent Mubali Jilala
akionesha Kitabu alichokiandika kijulikanacho kama “MWANZO WA KUWA
TAJIRI “ambacho kimezinduliwa leo na Mhashamu Askofu wa Kanisa
Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu katika Ibada ya Sakramenti
ya Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu
John Mjini Bariadi.

Mhashamu Askofu wa Kanisa
Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiingia katika Kanisa
Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi ambapo aliongoza Ibada
ya Sakramenti ya Kipaimara.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka (mwenye shati jeupe) na Mkewe Neema Mbiha(kulia)
wakifuatilia mahubiri wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika
Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi iliyoongozwa na
Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu.

Vijana wa Kipaimara (wenye sare ya
rangi nyekundu) katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini
Bariadi wakiingia Kanisani kwa ajili ya ibada ya Sakramenti hiyo,
ambayo iliongozwa Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la
SHINYANGA Liberatus Sangu.

Mhashamu Askofu wa Kanisa
Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akizindua Kitabu cha
“MWANZO WA KUWA TAJIRI” wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara
katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi,
kilichoandikwa na Muumini wa Kanisa hilo Ndg.Vincent Mabula Jilala.

Mhashamu Askofu wa Kanisa
Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu (katikati), Paroko wa
Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi Padre Kizito Nyanga na Mapadri
wengine wakifuatilia Ujumbe wa Mkuu wa Mkoa wakati wa Ibada ya
Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John
Mjini Bariadi.
…………………………
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mhashamu Askofu wa Kanisa
Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu amewataka Vijana kutokubali
kutumiwa kuleta vurugu, chuki na mafarakano hapa nchini.
Askofu Sangu ametoa wito huo
wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa
Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
“……Maandiko Matakatifu yanasema
Vijana wana nguvu; kwa hiyo nawasihi vijana popote pale mlipo muwe
chimbuko la Upendo, furaha na amani; watu wengine wasitumie nguvu zenu
vijana kuleta chuki, fitina na mafarakano, muwe macho” alisema Askofu
Sangu.
Askofu Sangu amewaasa waumini wa
Kanisa hilo kuishi maisha mema ambayo hayatakuwa chanzo cha mateso kwa
watu wengine katika familia, jumuiya , jamii wanaoishi na Taifa kwa
ujumla.
Aidha, amewataka Watanzania wote
kupinga na kukemea mauaji ya watu wenye ualbino kwa kuwa wanayo haki ya
kuishi kama watu wengine na watu wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa Kanisa kuwa na mtazamo wa
kuisaidia nchi katika kupambana na tatizo la ajira hususani kwa vijana.
Ameongeza kuwa ni vema Kanisa
liyavae maneno ya Mhe.Rais kuhusu Ujenzi wa Tanzania ya Uchumi wa Kati
na kuona namna linavyoweza kushiriki katika kufikia Tanzania Mpya, kwa
kuimarisha Idara za Kanisa na Vyama vya Kitume na kuzijenga idara na
vyama hivyo katika mtazamo wa Kiujasiriamali.
“Kanisa lione namna gani WAWATA
tulionao wanakuwa WAWATA wa miradi, VIWAWA wanakuwa wa miradi, TYCS wa
miradi, lakini sasa Vyama vyetu vya Kitume navyo pia vianze kujielekeza
kusaidia Kanisa kwenye eneo la miradi”amesema Mtaka.
Mtaka amesema upo umuhimu wa
kufanya semina za Ujasiriamali kwa vijana, wanawake na Vyama vya Kitume
katika Kanisa na waumini wote kwa ujumla ili kuwa na waumini
waliojengwa kiuchumi na wanaoendana na mtazamo wa Serikali ya Awamu ya
Tano ya kufikia Uchumi wa Kati.
Akiwa katika Ziara yake Mkoani
Simiyu, Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA
Liberatus Sangu , Jumamosi Septemba 02 alizindua Parokia mpya ya
Mtakatifu Luka iliyopo Mjini BARIADI, sambamba na kutoa kipaimara na
leo ametoa kipaimara kwa vijana 164, katika Kanisa Katoliki Parokia ya
Mtakatifu John Mjini Bariadi.
SHARE
No comments:
Post a Comment