Watu wanne
walijeruhiwa, watatu kati yao vibaya, baada ya gari kugonga ukuta na
kuingia hadi ndani ya nyumba eneo la York nchini Uingereza.
Gari hilo aina ya VW Golf lilifika hadi sebuleni na kumjeruhi dereva, abiria wawili na mwanamume mmoja aliyekuwa akipumzika kwenye kochi.
Gari hilo liliingia hadi sebuleni na kumjeruhi mwanamume aliyekuwa akipumzika kwenye kochi
Sajini Paul Cording wa kikosi cha polisi cha Yorkshire Kaskazini alisema ni "jambo la kushangaza kwamba hakuna aliyefariki".
Mwanamume mmoja ambaye anaaminika kuwa dereva wa gari hilo, ambaye ana miaka 20 hivi, alikamatwa.
Sajini Cording alisema gari hilo ni kama "liliingia ndani ya nyumba hiyo katika barabara ya Rivelin Way, mtaa wa Clifton Moor.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment