Alvaro Morata na
David Silva walikuwa miongoni mwa waliotikisa wavu viongozi wa Kundi G
Uhispania walipolaza Liechtenstein 8-0 katika mchezo wa kufuzu Kombe la
Dunia.
Alvaro Morata alijiunga na Chelsea kutoka Real Madrid majira ya joto
Kiungo wa kati wa Manchester City Silva aliongeza la nne kabla ya Iago Aspas kufanya mambo kuwa 5-0.
Iago alimsaidia Morata kufunga lake la pili kisha mwenyewe akajifungia bao lake kabla ya Max Goppel kujifunga dakika za mwisho na kukamilisha ushindi huo.
Uhispania wanaongoza Kundi G wakiwa na alama tatu na wameongeza tofauti yao ya mabao hadi 29, mabao 17 zaidi ya Italia walio wa pili na ambao walilaza Israel 1-0 Jumanne.
SHARE









No comments:
Post a Comment