Aliyekuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene (kushoto
mbele) akisaini mkataba na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi wakisaini mkataba wa makadhiano ya eneo ya la
Jeshililipo Ihumwa lilikokabidhiwa kwa Serikali kwa ajili ya matumizi
mbalimbali.
Makabidhiano
yakifanyika mbele ya viongozi wa Serikali na wananchi ni aliyekua
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene (kushoto
mbele) akikabidhiwa nyaraka za makabhiano na Waziri wa Ulinzi na Jeshi
la kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi wakati wa makadhiano wa eneo
la Ihumwa lenye ukubwa wa Hekta 752.
Aliyekuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene (Pili Kulia)
akikabidhi nyaraka za makabidhiano ya eneo la Ihumwa kwa Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana .
Aliyekuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene (aliyesimama)
akizungumza na viongozi na wananchi wakati wa makadhiano ya lililokuwa
eneo la Jeshi Ihumwa.
Baadhi wa viongozi na walioshiriki kwenye makabidhiano ya lililokuwa eneo la Jeshi Ihumwa.
………………..
Nteghenjwa Hosseah, Tamisemi – Dodoma.
Jeshi la Wananchi wa Tanzania
limekabidhi eneo la Ekari 1,855 sawa na Hekta 752 lililopo kwenye Kambi
ya Ihumwa Mkoani Dodoma kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene ili liweze
kutumika kwa ujenzi wa Ofisi za Serikali.
Akikabidhi eneo na nyaraka
zinazohusika Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Hussein
Mwinyi amesema eneo linalokabidhiws limegawanyika katika ameneo makuu
matatu ambayo ni eneo Na.4 lenye ukubwa wa Ekari 699.9 ambalo ndio
eneo halali la Jeshi na Nyaraka za Uthamini kwa ajili ya eneo Na.5
ambalo bado halijalipwa Fidia ya Tsh Bil 1.4 kwa wananchi wa kijiji cha
Mtuma.
Pia aliongeza kuwa makabdhiano
hayo pia yanahusisha Nyaraka za uthamini wa eneo Na. 2 lenye ukubwa wa
Ekari 304 ambalo bado halijalipwa Fidia ya Tsh Mil 866 kwa wananchi wa
Kijiji cha Mahoma Makulu.
Amesisitiza kuwa baada ya
makabidhiano haya Mamlaka zinazohusika zichukue jukumu la kupima upya
Eneo la Jeshi, eneo la barabara na eneo linalokabidhiwa ili kubainisha
na kuweka mipaka halisi ya kila eneo.
Akipokea eneo na nyaraka hizo
aliyekuwa Waziri wa Tamisemi Mhe. Simbachawene ameshukuru Jeshi la
Wananchi wa Tanzania kwa uamuzi wa kizalendo wa kutoa eneo hilo kwa
maslahi mapana ya Serikali na Wananchi kwa ujumla.
“Eneo hili tunalolipokea leo
litasaidia sana wakati huu ambao Serikali inahamia Dodoma na inahitaji
maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya Serikali hivyo uongozi wa
Mkoa pamoja na Halmashauri msimamie ipasavyo ili malengo tuliyojiweka
yaweze kufikiwa kwa haraka na ufanisi wa hali ya juu” Alisema Mhe.
Simbachawene.
Pia aliwaagiza viongozi wa
Manispaa ya Dodoma waingilie kati na kudhibiti uuzaji holela wa maeneo
katika Mji wa Dodoma unaokua kwa kasi ili kuzuia migogoro kati ya
Serikali na Wananchi lakini pia wananchi na wananchi inayoweza kujitokea
hapo baadae.
“Nimekuwa nikishuhudia na kuona
watu kutoka maeneo ya mbali wakija kununua viwanja na mashamba makubwa
katika Mji wa Dodoma naomba msimamie hili kwa sababu maeneo mengine
yamekwisha fanyiwa uthamini na wamiliki kulipwa Fidia lakini kwa sababu
bado hakujaendelezwa wananchi wale wanauza tena maeneo hayo kwa watu
wengine hii inaweza kuleta athari kubwa hapo baadae”
Aliyekuwa Waziri wa Tamisemi Mhe.
Simbachawene amekabdhi eneo hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordani
Rugimbana ambaye naye alikabidhi kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Dodoma Mhe.Prof. Davis Mwamfupe sambama na Mkurugenzi Ndg.Godwin
Kunambi.
SHARE
No comments:
Post a Comment