Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na
ujumbe kutoka Malawi ambao umetembelea hospitali hiyo LEO ili kujifunza
jinsi inavyoboresha huduma za afya. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya nchini Malawi, Dk. Dan Namarika.
Ujumbe kutoka Malawi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Museru.
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Muhimbili, Dk Julieth Magandi akieleza muundo wa hospitali kwa ujumbe wa Malawi.
Wakurugenzi wa Muhimbili wakiwamo watalaamu wengine wa afya wakimsikiliza Dk Magandi leo.
Ujumbe wa Malawi ikiongozwa na wenyeji wao wakiwa katika Jengo la Watoto leo.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali (EMD), Dk Juma Mfinga akitoa ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na idara hiyo.
Ujumbe kutoka Malawi ukiwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili.
………………………
Dar es salaam
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea ujumbe wa wataalamu wa Afya kutoka Wizara ya Afya ya nchini Malawi.
Ujumbe
huo umeongozwa na Katibu wa Afya nchini humo , Dk. Dan Namarika
umehusisha Madaktari , viongozi pamoja na wataalam mbalimbali kutoka
katika Wizara hiyo pamoja na taasisi nyingine za afya .
Akizungumza
jana baada ya kupokea ujumbe huo , Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru amesema ujio wa watalaamu hao
unatoa fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi.
Naye
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Dk. Juliethi Magandi amesema katika mwaka wa Fedha 2016-2017
Hospitali imehudumia wagonjwa wa nje 436, 394 wakati wagonjwa wa ndani waliohudumiwa
ni 59,555.
Akizungumzia
lengo la ujio wao , Katibu wa Afya wa nchi hiyo Dk. Dan Namarika
amesema wamekuja kujifunza jinsi ambavyo MNH inafanya kazi na
kutekeleza mipango yake .
Lengo
la serikali ya Malawi na Wizara ya Afya kwa ujumla ni kuhakikisha
inaboresha utoaji wa huduma hususani katika Hospitali za Umma nchini
humo.
Ujumbe
usema kuwa umefurahishwa jinsi Muhimbili inavyotoa huduma za kibingwa
na kusomesha wataalamu wa afya nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa
mafunzo.
SHARE
No comments:
Post a Comment