SPIKA Mstaafu ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne
Makinda, amewataka watanzania kutumia Mfuko wa Taifa wa Bima hiyo ili kupata unafuu
wa matibabu pindi wanapougua.

Wito huo alitoa
jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti huyo wakati alipozindua kitengo cha
kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo katika Hospitali ya Kairuki.

Alisema, kutokana
na gharama ya matibabu kupanda kila siku,kadi za bima ya afya zitasaidia kwa kiasi kikubwa
kupata unafuu wa matibabu kipindi mgonjwa anapokuwa hana fedha.

Makinda,
alisema bima hiyo inatoa fursa kwa wanachama kupata huduma za matibabu katika
hospitali wanazoona zinatoa huduma nzuri na kumjali mgonjwa.

“Vituo vyenye
huduma ya NHIF vinapaswa kutibia wagonjwa kwa kuwajali , kuwapenda pamoja na
kuwa wakarimu kwa wagonjwa kwani huduma hii inasaidia sana watu hasa wale
wanaougua magonjwa yenye kulipia gharama
kubwa,”alisema Makinda.

Aidha alisema ni watu wachache ambao wanauwezo
wa kujitibu bila bima ya afya lakini watu wengi wanategemea huduma hiyo
kulingana na gharama kubwa za matibabu katika baadhi ya magonjwa.

Kwa Upande
wake Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki Dk. Asser Mchomvu, alisema nchini Tanzania
watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa
yanayosababishwa na matatizo ya figo.

“Kwa hivi sasa
ugonjwa huo umeonekana kuathiri kati ya
asilimia 7 hadi 13 ya watanzania, wengi wao wakiwa wagonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus)na shinikizo la
damu(Acute Kidney injury) ,”alisema.

Alisema kwa
muda mrefu hospitali yao imekuwa
ikipokea wagonjwa wenye matatizo ya figo na kulazimika kuwapa rufaa kwenda nje
ya hospitali hivyo kupitia kitengo hicho kitaweza kutibu wagonjwa 40 kwa siku.

Alisema kuwa
kutakuwa na mashine 10 zenye uwezo wa kuwahudumia wagonjwa na hadi
kufikia sasa wamepata kibali cha wizara husika ambapo miongoni mwa mashine hizo
ipo ya kuchuja damu itakayosaidia kuzuia
uharibifu wa figo wa kudumu na wa muda hivyo kuokoa gharama.

Dk. Mchomvu,
alisema hospitali hiyo inatarajia kuongeza idadi ya mashine ili kuweza kuwahudumia
wagonjwa wengi pamoja na kutoa huduma ya
kupandikiza figo na kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo.

Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHJF), Anne Makinda
(katikati), akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki Hospitali,
Kokushubila Kairuki (kushoto), wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha kuchuja
Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Kairuki Hospitali.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kairuki Hospitali Dk. Asser Mchomvu, akitoa hotuba yake wakati
wa uzinduzi wa Kitengo cha kuchuja Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya
figo cha Kairuki Hospitali.
Baadhi ya madaktari waliohudhuria hafla hiyo wakisikiliza hotuba za viongozi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki Hospitali, Kokushubila Kairuki akitoa hotuba yake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda (kushoto), akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha Kuchuja Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijjini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki, Kokushubila Kairuki.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda (kushoto), akipata maelezo alipotembelea kitengo cha kuchuja damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo.
Dk. Muga akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Muuguzi wa Kitengo cha Kuchuja Damu, Eva Beatus.
Jengo la Kitengo hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda, akitoa hotuba yake.

SHARE
No comments:
Post a Comment