Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group, Roberto Jarrin (kulia) akimkaribisha
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles
Kichere wakati alipoongoza ujumbe wa Maofisa Waandamizi wa taasisi hiyo
katika ziara ya kikazi katika kiwanda cha Bia cha Tanzania Breweries
Limited, kilichopo Ilala jijini Dar e Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group, Roberto Jarrin (aliyesimama)
akielezea ujumbe wa Kamishna Mkuu wa TRA utendaji kazi wa kampuni hiyo.
Meneja wa Afya na Usalama sehemuya kazi wa TBL Group, Renatus
Nyanda (kushoto) akimweleza Kamishna Mkuu wa TRA (Kulia) na ujumbe wake
utekelezaji wa kanuni za usalama wa kampuni kabla ya kuanza ziara ya
kutembelea kiwanda ,wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL,Roberto
Jarrin.
Kamishna
Mkuu wa TRA na ujumbe wake wakipata maelezo ya mchakato wa kutengeneza
bia kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha TBL cha Ilala-Calvin Martin.
Mtaalam
wa kuonja bia wa TBLGroup, Rebecca Semoka, (kushoto) akimweleza
Kamishna Mkuu wa TRA na ujumbe wake mchakato wa kuonja ubora wa radha ya
bia kabla ya kuingia kwenye masoko.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TBL Group,Roberto Jarrin ( wa nne kulia) na Kamishna Mkuu
wa Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA) Charles Kichere ( wa tatu kushoto )
wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Waandamizi wa TBL na TRA wakazi
wa ziara ya kikazi ya watendaji wa TRA katika kiwanda hicho.
SHARE
No comments:
Post a Comment