Na Veronica Simba – Geita
Kamishna
wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, ameshuhudia na
kushiriki katika zoezi la kuhakiki na kufunga madini ya dhahabu katika
Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya
nchi.
Kamishna
Mchwampaka alishiriki zoezi hilo hivi karibuni, akiwa katika ziara ya
kazi mkoani Geita kukagua shughuli mbalimbali za sekta ya madini.
Zoezi
la uhakiki na ufungaji wa dhahabu inayosafirishwa, hufanyika katika
chumba maalum kijulikanacho kama gold room kilichopo mgodini na
hushirikisha maafisa mbalimbali wa Serikali kutoka Jeshi la Polisi,
Wizara ya Nishati na Madini na Mamlaka ya Mapato Tanzania pamoja na
maafisa wa Mgodi.
Akizungumzia
lengo la maafisa wa Serikali kutoka sekta husika kushiriki katika zoezi
hilo; Kamishna Mchwampaka alieleza kuwa ni kwa Serikali kujiridhisha na
thamani ya dhahabu inayosafirishwa ili kuhakikisha inapata mapato
stahiki na kuepusha udanganyifu wowote unaoweza kujitokeza.
“Katika
hili, tuko imara na makini. Ni lazima tuhakikishe kuwa Serikali inapata
mapato stahiki kulingana na dhahabu inayosafirishwa. Ndiyo maana unaona
maafisa wetu kutoka sekta zote muhimu wanashiriki kikamilifu katika
zoezi hili.”
Aliwataka
watanzania kuondoa hofu na kuiamini Serikali ya Awamu ya Tano
inayowaongoza kuwa iko makini na imejipanga kusimamia kikamilifu maslahi
ya wananchi.
Kamishna wa Madini yuko katika ziara ya kazi Kanda ya Ziwa kukagua shughuli mbalimbali za sekta husika.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mwenye koti), akihakiki uzito wa Mkuo wa Dhahabu, katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kabla ya kufungwa na kusafirishwa nje ya nchi. Wengine pichani ni baadhi ya maafisa wa Serikali na GGM.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mwenye koti-kulia), akishuhudia Mkuo wa Dhahabu wenye uzito wa kilogramu 26, ukiwekwa ndani ya mfuko maalum kabla ya kufungwa kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi. Wengine pichani ni baadhi ya maafisa wa Serikali na GGM.
Afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Anuari Fadhili akiweka ‘seal’ maalum ya Serikali kwenye Kasha lenye Mkuo wa Dhahabu baada ya ukaguzi katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi. Wanaoshuhudia ni Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati) na maafisa wengine wa Serikali na GGM.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati), akitoa maelekezo kwa maafisa wa Serikali pamoja na wale wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kuhusu zoezi la uhakiki na ufungaji dhahabu inayosafirishwa nje ya nchi.
Kasha lenye Mkuo wa Dhahabu katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), lililohakikiwa na kufungwa tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati) na timu yake, wakiondoka ndani ya eneo la Mtambo/kiwanda cha kuchakata dhahabu katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), baada ya kushiriki zoezi la uhakiki na ufungaji wa dhahabu inayosafirishwa nje ya nchi. Pamoja nao ni maafisa wa GGM.
SHARE
No comments:
Post a Comment