Kampuni
ya Namaingo Business Agency Co. Ltd imezindua Mradi mkubwa wa ufugaji
kuku unaosimamiwa na Kikundi cha Ujasiriamali cha Shinyanga,Kishapu na
Kahama (SHIKIKA) uliopo katika mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha katika
manispaa ya Shinyanga.
Uzinduzi wa mradi huo umefanyika leo Jumatatu Septemba 18,2017 katika mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha manispaa ya Shinyanga.
Kikundi
cha SHIKIKA kinachotekeleza mradi huo,kilianzishwa Machi 16,2017 baada
ya kampuni ya Namaingo Business Agency Co.Ltd kuwaelekeza wanachama wake
kuunda vikundi vya wanachama hamsini hamsini ili wakubaliane kuendesha
mradi wanaoupenda.
Wanakikundi
hao waliamua kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji ndipo
kampuni hiyo ikawachangia vifaranga 200,wakaanza ufugaji tarehe 9.6.2017
na mpaka sasa kikundi kina kuku zaidi ya 1300.
Akizungumza
wakati wa kuzindua mradi huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo
Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim aliwapongeza wanakikundi hao kwa
kuchangishana fedha shilingi milioni 8 na kuamua kuanzisha mradi huo.
“Ndugu
zangu jambo hili mlilofanya na mlilolitekeleza kwanza ni jambo la
kitaifa kwa sababu wananchi wakiwa na uchumi mzuri serikali nayo inapata
kodi lakini pia tunakuwa tumetengeneza ajira”,alisema Ibrahim.
“Pamoja
na jitihada hizi mlizochukua kwa muda mfupi,Tunatamani kuona kila mtu
anakuwa na kuku walau 1000 kwenye banda lake,najua changamoto kubwa
iliyopo ni mitaji na riba kubwa kwenye mikopo lakini kuna fedha kwa
ajili ya maendeleo ya akina mama na vijana zenye riba ndogo sana zipo
kwenye benki mbalimbali,serikali inafanyia kazi suala la mikopo hiyo”,aliongeza.
Aidha
Ibrahim aliwataka wananchi kuwa na maamuzi ya kutoka katika hali
walizonazo kwa kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa na kuilaumu
serikali.
“Hakuna
haja ya kuilaumu serikali bali unapaswa kujiajiri ili kubadilisha
maisha yako,hakuna maisha mazuri kama mtu ukijiajiri,hata hao
waliojiriwa wakistaafu huwa wanarudi kujiajiri hivyo kujiajiri ndiyo
kila kitu katika maisha yako”,aliongeza Ibrahim.
“Sisi
Namaingo Bussiness Agency Co. Ltd kazi yetu ni kuwabadilisha kiakili ili
muweze kubadilika kimawazo kwani fursa za kubadili maisha yenu,zipo
nyingi,kufanikiwa kwa mtu ni maamuzi ya mtu mwenyewe”,alisema.
Akisoma
risala, Katibu Msaidizi wa SHIKIKA,Beatrice Nangale alisema gharama za
kuanzisha mradi huo ni shilingi milioni 8 lakini mpaka sasa umegharimu
shilingi milioni 20 ambazo ni michango ya wanachama.
Alisema
ili kufikia malengo yao,kundi hilo linahitaji eneo kubwa la ekari 3000
kwa ajili kupanua mradi wa kuku,kuwa na mashine za kutotolea,kutengeneza
chakula cha kuku,kuchakata minofu ya kukuna ufugaji wa nyuki wa asali.
“Pia
tunataka kufuga samaki,mbuzi,sungura na ng’ombe kisha kusindika nyama
zao,kulima mboga mboga na matunda kama vile mapapai,kupanda miti na
kujenga nyumba kwa ajili ya makazi”,alifafanua Nangale.
Hata
hivyo alizitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni ukosefu wa
chakula na dawa za kuku mjini Shinyanga,masharti magumu ya benki za
utoaji mikopo,ukosefu wa wataalam wa masuala ya mifugo pamoja na kukosa
wahisani na misaada ya wahisani kutokana na hali ngumu za kiuchumi za
wanakikundi.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamaguha Deo Masalu alisema mradi
huo utatumika kama shamba darasa na kuahidi serikali kuwapa ushirikiano
wanachama wa kikundi ili kuhakikisha wanafikia malengo yao.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim
akijiandaa kukata utepe kwa ajili ya kuzindua mradi wa kuku unaosimamiwa
na Kikundi cha Ujasiriamali kutoka Shinyanga,Kishapu na Kahama
(SHIKIKA) leo Septemba 18,2017.Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1
blog
Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akikata utepe.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim
akishikana mkono na Katibu wa SHIKIKA,Gelard Egwaga baada ya kukata
utepe.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim
akiangalia kuku wenye umri wa miezi miwili katika moja ya mabanda ya
kundi la SHIKIKA.
Viongozi
wa kundi la SHIKIKA wakimwongoza Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo
Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim kuangalia kuku hao.
Ndani ya banda la kuku,mgeni rasmi Biubwa Ibrahi na waangalizi wa kuku (vijana watatu kulia).
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akiwa
amebeba jogoo mwenye umri wa miezi minne katika banda la kuku.
Kuku wakiwa katika banda.
Katibu wa SHIKIKA,Gelard Egwaga akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wao wa ufugaji kuku unaosimamiwa na SHIKIKA.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim
akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuku unaosimamiwa na SHIKIKA.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim
akisisitiza umuhimu wa kujiari badala ya kutegemea kuajiriwa na
serikali.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akizungumza.
Mwenyekiti wa SHIKIKA,Kiyungi Mohamed Kiyungi akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Wanachama wa SHIKIKA wakiwa eneo la tukio.
Wanachama wa SHIKIKA wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.
Uzinduzi wa mradi unaendelea.
Mratibu
wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd mkoa wa Shinyanga,Vaileth
Kyando akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ufugaji kuku.
Katibu Msaidizi wa SHIKIKA,Beatrice Nangale akisoma risala kwa niaba ya wanachama wa SHIKIKA.
Wa kwanza
kushoto ni Afisa Mtendaji wa kata ya Chamaguha,Deo Masalu,Mkurugenzi wa
Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim na Katibu wa
SHIKIKA,Gelard Egwaga wakifuatilia kwa umakini risala kutoka kwa Katibu
Msaidizi wa SHIKIKA,Beatrice Nangale.
Makamu mwenyekiti wa SHIKIKA,Aneth Muro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa ufugaji wa kuku.
Afisa
Mtendaji wa kata ya Chamaguha,Deo Masalu akizungumza wakati uzinduzi wa
mradi wa ufugaji kuku unaotekelezwa katika kata yake.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
SHARE
No comments:
Post a Comment