Na Tiganya Vincent-Nzega
Wakazi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa wametakiwa kujiepusha na
vitendo vya kishirikina na kuwa na hofu ya Mungu na hivyo kuachana na
mauaji ya watu mbalimbali wakiwemo wazee wenye macho mekundu, wakinamama
wanaohisiwa kuwa wachawi na watu wenye ulemavu.
Kauli hiyo imetolewa jana na
Mmiliki wa Studio ya Big D Entertainment na Mlezi wa Kwaya ya Watoto wa
Kanisa la African Inland Church(T) la Nzega mjini John Dotto wakati wa
uzinduzi wa Kanda ya Nyimbo za Mchungani Egon Israel yenye kubeba jina
la Nakuombea Jirani.
Alisema kuwa watu wanaomcha Mungu
na walioshika maagizo yake hawezi kuwaua wazee kwa sababu ya kuonekana
kuwa na macho mekundu yaliyotokana na uzee wao na wala hawezi kufirikia
kuwaua wenye ulemavu wa ngozi .
Doto alisema njia pekee ya kuondokana na aibu hiyo hasa kwa
mikoa ya Kanda ya ziwa ni kuhimiza watu wote kwa imani zao katika maeneo
hayo kuishi misingi ya dini yake na maelekezo ya Mungu yanayotolewa na
viongozi wa kiroho wakiwemo wachungaji, Masheikh na Makasisi.
Alisema kuwa inapotekea jambo lolote sio zuri katika maeneo
hayo kama vile ugonjwa na kifo baadhi ya wenyeji wamekuwa wakimbilia
katika kuamini kuwa wamerogwa na kuanza kuwasihi watu na kuchukua hatua
ambazo sio sahihi.
Katika kuhakikisha kuwa neno la
Mungu linawafikia watu wengi kwa njia ya nyimbo Doto aliahidi kuwa
tayari kuwazisaidia bure Kwaya zote za Kanisa hilo ambazo zitahitaji
kurekodi katika Studio yake nyimbo zinazotoa ujumbe wa neno la Mungu
kama sehemu ya kuhamasisha jamii kumcha Mungu na kuachana na aibu ya
kila mara mikoa ya kanda ya ziwa kunyoshewa vidole kwa ajili ya mauji
yanakuwa yamechangia kuamini ushirikina.
Doto alisema kuwa pesa wanazitumia
na nguvu wanazozitumia kuondoa maisha ya watu wasio na hatia zitatoa
ushahidi mbele ya Mungu siku ya hukumu na kuwaomba watu kutumia nguvu
zao na akili walizojaliwa kutafuta mali kwa njia halali.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Umoja
wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Regina Athuman alisema kuwa
jina la wimbo uliobeba mkanda la Nakuombe jirani linawataka Watanzania
kuishi kwa upendo na ushirikino.
Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia
kuwafanya kuachana na vitendo viovu na vinavyosababisha baadhi yao
kushawishika na kwenda kuwatendea maovu wazee na watu wenye ulemavu.
Akisoma risala wakati wa uzinduzi
wa albunu hiyo Katibu wa Kanisa la AICT –Nzega Walwa Milambo kwa niaba
ya mchungano Egon Israel alisema kuwa uzinduzi huo unalenga kupanua
huduma ya kiroho ikiwemo kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa na
ununuzi wa vifaa vya kurekodia nyimbo.
Alisema kuwa lengo ni kutaka watu
wengi wapate neno la Mungu kwa njia ya maubiri na nyingi ili waweze
kuondokana na matendo maovu na yanayorudisha nyuma maendeleo katika
jamii na Taifa kwa ujumla.
Katika uzinduzi huo wa albamu ya
Ninakuombea Jirani Mmimiliki wa Studio ya Big D Entertainment John Doto
alitoa milioni 1 na wadau wengine walichangia shilingi milioni 1.5
ambapo jumla ilikuwa milioni 2.5.
Mikoa ya Tabora, Shinyanga, Geita
na Mwanza imekuwa ni miongoni mwa maeneo ambayo watu wenye ulemavu wa
ngozi na wazee wanaripotiwa kutendewa unyama ikiwemo kuwaua.
SHARE
No comments:
Post a Comment