Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habaro ofisini kwake leo.
…………………………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI
ya Udalali ya Msama, imetangaza msako wa wezi wa kazi za sanaa kwa
ujumla wake ambao wamekuwa kikwazo cha wahusika kutofaidi matunda ya
ubunifu, jasho na kazi zao.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Udalali ya
Msama, Alex Msama alisema kazi hiyo ngumu na muhimu kwa maslahi ya
wasanii na Serikali, inaa siku yoyote kuanzia sasa.
Msama
alisema kutokana na wizi huo kuwanyonya wasanii pamoja na kuikosesha
Serikali pato lake halali kupitia kodi, kampuni yake imepewa jukumu hilo
kwa msaada wa Jeshi la Polisi.
“Naishukuru Serikali kwa kusikia kilio cha wasanii mbalimbali kuanzia wale wa muziki wa injili, Dansi, Bongo Fleva na hata wengineo, wamekuwa wakilia kazi zao kutajirisha wajanja,” alisema Msama.
Msama alisema kibaya zaidi ni kwamba, wizi huo wa kazi za sanaa sio tu umekuwa ukiwanyonya wasanii, pia ni kuinyima Serikali mapato halali kwa ajili ya kuzitumia kwa maendeleo ya nchi.
Alisema
kazi hiyo itakayofanywa na kampuni yake kwa ushirikiano wa karibu zaidi
na Jeshi la Polisi, utagusa mikoa yote ya Bara kwa kukamata wote wenye
kuuza kazi zisizotambulika kisheria.
“Hii
ni pamoja na kazi zote zisizo na stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), hivyo wenye kuuza CD, DVD feki pamoja na kunyonya kazi za wasanii
katika flash, wote hawatabaki salama,” anasema.
Alisema
ni heri wenye kujihusisha na kazi hiyo haramu, wakatafute kazi nyingine
halali kwani tayari wanayo majina, hivyo wanajua waanzie wapi siku na
saa ya kuanza kutoka mkoa mmoja hadi mwingine.
“Tunatangaza
kuwa, tunaingia kazini kusaka wote wenye kujipatia vipato kutokana na
ubunifu na jasho la wengine, huku wahusika wakibaki masikini. Msako huu
hautaacha mtu,” alionya Msama.
Mbali
ya ukurugenzi mkuu katika kampuni hiyo ya Udalali, Msama pia ndiye mdau
aliyechangia kukua kwa muziki wa injili kupitia uratibu wa matukio ya
Tamasha la Pasaka, Krismas ama uzinduzi wa kazi mpya.
Alisema
katika hatua ya awali, msako huo utakaokuwa chini ya Polisi wapatao 100
katika maeneo mbalimbali ya nchi, utaanzia jijini Dar es Salaam,
Morogoro na Dodoma.
SHARE
No comments:
Post a Comment