Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Maxcom Africa,Jameson Kasati akimkabidhi KADI ya MALIPO Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Mipango, Gerald Jeremiah wa hospitali
hiyo. Kadi hiyo itatumika kulipia huduma za afya katika hospitali hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na
waandishi wa habari Leo kuhusu mfumo wa kulipia huduma za afya kwa
kutumia kadi maalamu. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Maxcom
Africa,Jameson Kasati na kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Mipango,
Gerald Jeremiah.
Baadhi ya maofisa wa Muhimbili na
Maxcom Africa wakifuatilia mkutano huo Leo ambao umefanyika katika
hospitali hiyo. Wengine waliokaa nyuma ni waandishi wa habari
wakifuatilia mkutano huo leo.
Mkurugenzi wa Fedha na Mipango,
Gerald Jeremiah wa Muhimbili akitoa maelezo jinsi ya kulipia huduma za
afya kwa kutumia KADI ya Malipo ambayo imetengenezwa MNH kwa
kushirikiana na Muhimbili.
Baadhi ya maofisa wa Muhimbili wakifuatilia mkutano huo leo.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya Maxcom
Afrika, Deogratius Lazari akiwaeleza waandishi wa habari jinsi wagonjwa
na ndugu wa wagonjwa wanavyolipia huduma za afya kwa kutumia kadi
maalimu.
………………………..
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imezindua mfumo wa kulipia huduma za afya kwa kutumia kadi maalumu.
Huduma
hiyo tayari imeanza kutolewa na hospitali hiyo kwa kushirikiana na
Kampuni Maxcom Afrika ambayo imepokelewa vizuri na wagonjwa pamoja na
dugu wa wagonjwa.
Lengo
la kulipia huduma za afya kwa kutumia mfumo huo ni kupunguza muda
mwingi ambao wagonjwa wamekuwa wakitumia wakati wa kupatiwa huduma hizo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa
Lawrence Museru amesema MNH imekamilisha awamu ya kwanza ya usimikaji wa
mfumo wa malipo kwa njia ya kielekroniki kwa kutumia kadi maalumu ya
malipo au kwa kutumia simu za mkononi.
“Awamu
ya pili wagonjwa au ndugu wa wagonjwa wataanza kulipia huduma za afya
kupitia kadi zao za benki aina ya viza au Mastercard. Pia, hospitali
itaongeza wigo wa kulipia kwa njia ya simu za mkononi kwa kupitia
mitandao ya TTCL Pesa, Halopesa na Easypesa,” amesema Profesa Museru.
Malipo kwa njia ya Kadi Maalumu (Muhimbili Card)
(i) Mgonjwa au jamaa wa mgonjwa atapewa Kadi Maalumu na Wakala wa Muhimbili (Maxcom) ambapo atatakiwa kuijaza fedha.
(ii)
Baada ya kujaza fedha kwenye Kadi, mgonjwa ataelekea eneo la kutolea
huduma na atapewa Hati ya Gharama (Bill Note) na kutakiwa kulipa.
Atatumia Kadi yake kwa kuigusisha katika mashine ndogo (POS) na mashine
hiyo itakata kiasi kilichooneshwa katika Hati ya Gharama na kutoa risiti
ya mashine.
(iii)
Mgonjwa ataendelea kutumia Kadi yake kulipia gharama na endapo fedha
kwenye Kadi zitakwisha atarudi kwenye dirisha la Wakala na kujaza tena
fedha. Ikiwa fedha zitabaki kwenye Kadi Mgonjwa atakuwa na hiari ya
kuziacha kwenye Kadi kama akiba au kuomba arejeshewe fedha taslimu.
Malipo kwa MPESA, TIGOPESA na Airtel Money
Wakati
Mgonjwa atakapopewa Hati ya Gharama (Bill Note) na akiamua kuchagua
kulipia kwa kutumia simu yake atafuata utaratibu ufuatao:
A. Kwa mfano MPESA, mteja ataanza kwa kubonjeza
*150*00#;
B. Baada ya hapo atachagua huduma namba 4 ‘’LIPA kwa M-Pesa’’;
C.
Baada ya hapo atachagua huduma namba 4 ‘’Weka namba ya Kampuni ‘’,
ambapo mgonjwa atajaza namba 356666 ambayo ni namba ya Hospitali ya
Taifa Muhimbili;
D.
Baada ya hapo mgonjwa atatakiwa kuweka namba ya kumbukumbu ya malipo.
Hapa mgonjwa atajaza namba iliyopo kwenye Hati ya Gharama (Bill Note)
ambayo ni ‘’Mobile Request Number’’;
E.
Mgonjwa atapata ujumbe kupitia simu yake ikimtaarifu kuwa muamala wake
umekamilika na fedha zimetumwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kwa
mitandao yote ya simu mgonjwa atafuata taratibu zote hapo juu baada ya
kubonyeza *150*01# kwa mteja wa Tigopesa na *150*60# kwa mteja wa
AirtelMoney.
SHARE
No comments:
Post a Comment