Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt
Rehema Nchimbi akisalimiana na Mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara
wateja wa NMB Singida Emmanuel Rweyemamu Kyoma mapema leo kabla ya
kufungua warsha ya siku moja ya klabu hiyo, katika ukumbi wa Kanisa
Katoliki mjini Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt
Rehema Nchimbi akikagua baadhi ya bidhaa za wafanyabiashara wateja wa
NMB Singida mapema leo kabla ya kufungua warsha ya siku moja, katika
ukumbi wa Kanisa Katoliki mjini Singida.
Meneja wa NMB Kanda ya kati
Straton Chilongola akizungumza klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB
Singida mapema leo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja, katika
ukumbi wa Kanisa Katoliki mjini Singida.
Wafanyabiashara wateja wa NMB
Singida wakiwa katika warsha ya siku moja katika ukumbi wa Kanisa
Katoliki mjini Singida mapema leo.
………………………………………………………………………
Benki ya NMB imetakiwa kuwasaidia
wafanyabiashara Mkoani Singida kuanzisha kiwanda cha kutengenea
vifungashio, ili waweze kuhifadhi bidhaa zao katika ubora unaokubalika
kitaifa na kimataifa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt
Rehema Nchimbi ametoa rai hiyo mapema leo wakati akifungua warsha ya
siku moja ya klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB, katika ukumbi wa
Kanisa Katoliki mjini Singida.
Dkt Nchimbi amesema klabu hiyo ya
wafanyabiashara itaweka alama kubwa katika maendeleo endapo watajipanga
na kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vifungashio hivyo kuliko kuendelea
kuvifuata nje ya Singida au nje ya nchi.
“Uzoefu usipotumika vizuri
unaweza ukawa kikwazo cha kuendelea, msizoee kufuata vifungashio na
label nje ya singida wakati fursa ipo ya kuanzisha kiwanda hicho
Singida”, amesema na kuongeza kuwa,
“Wafayabiashara mzipende biashara
zenu na kuziweka katika hali ya usafi na yenye kuvutia, wengine
wanapenda kujisafisha na kujipendezesha wenyewe lakini ukiangalia
biashara zao hazivutii, zimewekwa tu bila kufungashwa vizuri”,
amesisitiza.
Aidha amewataka wafanyabiashara
wasiogope kukopa kwakuwa sio jambo la aibu wala fedheha, ila
kinachotakiwa ni kuwa na nidhamu ya mkopo na malengo ili waweze
kufanikiwa.
“Akina mama jifunzeni kuwa na
nidhamu ya mkopo, sio unakopa leo mara unasikia kapu la mama, jifikirie
hayo ndio malengo ya huo mkopo hata kama ni jambo muhimu?, nidhamu ya
mkopo inatakiwa ianze kabla ya kukopa na iendelee kuwepo.
Dkt Nchimbi pia ameishukuru benki
hiyo kwa kushirikiana na serikali katika mambo mbalimbali ya kielimu na
afya, pia amewashukuru kwa kutoa mikopo kwa watumishi wa umma jambo
ambalo linawasiadia katika mambo mbalimbali.
Naye Meneja wa NMB Kanda ya kati
Straton Chilongola amesema klabu za wafanyabiashara nchini ziko 34
ambazo zimekuwa zikipatiwa mafunzo mikopo kutoka katika benki hiyo.
Chilongoloa amesema benki hiyo
imekuwa ikitoa mafunzo juu ya ulipaji kodi, ujasiriamali, masuala ya
mitaji, leseni na ardhi ili wafanyabiashara hao waweze kukuza mitaji
yao.
Amesema benki hiyo imefanikiwa
kuwakuza wafanyabiashara wengi ambazo wameanza nao wakiwa
wafanyabiashara wadogo ambapo sasa wamekuwa wakubwa na wakati huku
wakiajiri wengine na hivyo kukuza uchumi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB Singida Emmanuel Rweyemamu Kyoma
amesema wazo la kuanzisha kiwanda cha kutengeza vifungashio wamelipokea
vizuri huku wakijipanga kuandaa andiko kwa ajili ya kiwanda hicho.
Kyoma amesema kwa ushirikiano na
NMB kiwanda hichokitaweza kujengwa Singida huku wakimuahidi Mkuu wa Mkoa
kuwa Mkoa wa Singida utazalisha chakula cha kutosha kulisha Mkoa wa
Dodoma.
Amesema benki ya NMB imekuwa
ikishirikiana na wafanyabiashara hao hivyo mipango ya kukuza uchumi kama
huo wa kuanzisha viwanda utatekelezeka bila matatizo yoyote.
SHARE
No comments:
Post a Comment