Mkuu wa Mkoa wa Mbeya – Amos
Makalla (katikakati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa
tawi jipya la Nmb Uyole lililopo Jijini Mbeya. Ufunguzi wa tawi hili
unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa mikoa ya kanda ya Nyanda za juu
yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya – Amos
Makalla akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la NMB Uyole
uliofanyika jijini Mbeya. Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi
ya NMB 31 kwa mikoa ya kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa,
Iringa, Njombe, Songwe na Katavi.
Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani –
Augustino Mbogella akizungumza na wateja wa NMB waliokusanyika
kushuhudia uzinduzi wa tawi la NMB Mkwajuni wilayani Songwe katika mkoa
wa Songwe. Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa
mikoa ya kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe,
Songwe na Katavi.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Songwe na
Mkuu wa Wilaya ya Songwe – Samwel Jeremiah akikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Mkwajuni wilayani Songwe, wengine katika
picha (kutoka kushoto) Meneja wa NMB kanda ya Nyanda za Juu – Badru
Iddy, Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa ndani wa NMB – Augustino Mbogella, Mbunge
wa Jimbo la Songwe – Philipo Mulugo, Katibu Tawala wa wilaya ya Songwe –
Johari Samizi na Meneja wa Benki NMB Tawi la Mkwajuni – Michael Mzinga.
Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa mikoa ya
kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na
Katavi.
…………………………
BENKI ya NMB Imefungua matawi
saba kwa mpigo katika mikoa sita ikiwa ni juhudi za kujiimarisha zaidi
na kuwa karibu na Wateja wake wa kanda ya nyanda za juu.
Matawi hayo yamefunguliwa katika
mikoa ya Njombe, Mbeya,Songwe, Rukwa na Katavi. Matawi ambayo
yamefunguliwa na yanatoa huduma kwa jamii ni pamoja na NMB Kasumulu,
NMB Uyole, NMB Mkwajuni, NMB Wanging’ombe, NMB Laela na NMB Kalambo
lililopo Mlele.
Idadi hii ya matawi mapya
inafanya jumla ya matawi ya NMB 31 katika kanda ya Nyanda za Juu huku
yakifikia matawi ya NMB 207 nchi nzima.
Akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa Tawi la NMB Uyole lililopo mkoani Mbeya, Meneja wa Kanda ya
Nyanda za juu – Badru Iddy amesema kuwa lengo la Benki hiyo ni kusogeza
huduma zaidi kwa wananchi ili kuwa karibu na wateja wake.
“Kuzinduliwa kwa tawi hili la
NMB Uyole mahali hapa kunafuatia mahitaji ya muda mrefu ya wateja wetu
wa Uyole kupata tawi la NMB lenye nafasi ya kutosha .Aidha eneo hili ni
karibu zaidi na wafanyabiashara wengi ambao ni wateja wetu wakubwa na
wananchi kwa ujumla. Tawi hili kama yalivyo matawi yetu mengine nchini
linatoa huduma zote za kibenki zitolewazo na benki yetu,” alisema Badru
.
Akizungumza wakati wa uzinduzi
wa tawi la Uyole, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya – Amos Makalla alisema kuwa
Wananchi wanapaswa kufungua akaunti katika Benki hiyo na kuitumia kwa
kuwa serikali ina hisa ya asilimia 32 katika Benki hiyo.
“Hapa tuelewane, Serikali na
Benki ya NMB ni sawa na mapacha kwa kuwa kila mahala ambapo serikali
imepeleka huduma zake za kijamii Benki hiyo hufuatia kwa kuweka huduma
za kifedha ili kuwahudumia wananchi wa eneo husika,” alisema Mheshiwa
Makalla.
Huko Mkoani Songwe Mkuu wa
Wilaya ya Songwe – Samwel Jeremiah ambaye alimwakilisha mkuu wa Mkoa
huo – Chiku Galawa kwenye uzinduzi wa tawi la NMB Mkwajuni, aliwataka
wananchi kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha na hivyo kutumia fursa
zinazotokana na benki ya NMB kukuza uchumi wao na mwisho kuchangia
ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa ujumla. Alisema desturi ya kuhifadhi fedha
Benki kunajenga nidhamu ya matumizi ya fedha kuepuka madhara ambayo
yanaweza kutokea.
Awali akizungumza wakati wa
uzinduzi wa Benki ya NMB Tawi la Mkwajuni, Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa
Ndani – Augustino Mbogella alisema kuwa mkakati wa kibiashara wa NMB ni
kuhakikisha watanzania wengi zaidi wanapata huduma za kifedha na ndio
maana kila wilaya benki hiyo inafungua matawi ili kusogeza zaidi huduma
kwa wanannchi.
Alisema kuwa NMB ni benki ya
wananchi na wanatakiwa kuitumia kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla kwa
kupata huduma zote za kibenki ikiwemo mikopo ya kibiashara katika ngazi
mbalimbali.
“Benki ya NMB imeendelea kuwa
benki yenye mtandao mpana wa matawi na ATM kuliko benki nyingine yoyote
hapa nchini kwa kuwa na matawi zaidi ya 200 huku ikiwa na mashine za
kutolea fedha (ATM machines) zaidi ya 700 nchi nzima na Wateja zaidi ya
Milioni 2 na laki 5.
Mbogella aliongeza pia kuwa
“Benki yetu pia inatoa huduma zote zinazotakiwa kutolewa na benki yeyote
ya biashara nchini, tuna akaunti mbali mbali za akiba, huduma za mikopo
yenye masharti nafuu kwa ajili ya mahitaji yote kwenye soko, huduma za
fedha za kigeni, kukusanya mapato na kulipa kwa niaba ya serikali na
taasisi mbalimbali”.
SHARE
No comments:
Post a Comment