RAIS KARIA AUNDA KAMATI YA TUZO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameunda Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/18.
Kamati hiyo itaongozwa na
Mwenyekiti Ahmed Mgoyi wakati Makamu Mwenyekiti ni Almas Kasongo
ilihali Amiri Mhando ameteuliwa kuwa Katibu wa kamati hiyo ya tuzo.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
VIINGILIO MCHEZO WA AZAM FC v SIMBA SC
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania linapenda kuwatangazia wananchi kuwa viingilio katika mchezo wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Azam na Simba.
Mchezo huo utafanyika Uwanja wa
Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam na viingilio vitakuwa shilingi elfu
kumi (Sh 10,000) kwa Jukwaa Kuu ambalo lina uwezo wa kubeba mashabiki
1,000 tu walioketi, wakati mzunguko (popular) kiingilio kitakuwa ni
shilingi elfu saba tu (Sh 7,000).
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo
MATOKEO YA USAILI KWA WANAOGOMBEA TPLB
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepitisha majina ya wagombea wafuatao
kuwania uongozi katika nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Kamati ya
Uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu.
Majina hayo yamepitishwa mara
baada ya kuwafanyia usaili uliofanyika Jumapili Septemba 3, mwaka huu
kwenye Ukumbi wa TFF, Dar es Salaam. Uchaguzi Mkuu wa Kamati ya Uongozi
wa Bodi ya Ligi utafanyika Oktoba 15, mwaka huu.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo
LIGI YA WANAWAKE KUANZA NA LIGI NDOGO
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), limeagiza Makatibu wa Vyama vya Mikoa kutuma haraka
majina ya timu mabingwa wa mikoa wa soka la wanawake wa msimu wa
2016/17.
Viongozi wa mikoa wamekumbushwa
kutuma timu ili kufanya maandilizi ya haraka ya Ligi Ndogo
itakayofanyika Septemba 22 hadi 29, mwaka huu.
SHARE
No comments:
Post a Comment