TRA

TRA

Saturday, September 16, 2017

RC MAKONDA ARIDHISHWA NA UKARABATI WA MAGARI YA POLISI MKOA WA DAR ES SALAAM

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

 

POL1
Askari Polisi wakiwa tayari kwa kazi katika moja ya magari 18 yaliyokamilika kwa ukarabati kati ya magari 26 yaliyopelekwa kwenye gereji ya RSA mjini Moshi na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kwa matengenezo makubwa wakati alipoyakagua Septemba 15, 2017 mkoani Kilimanjaro.
POL2
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akikagua moja ya magari 18 kati ya 26 ya polisi Dar es salaam yaliyopelekwa mjini Moshi katika gereji ya RSA kwa matengenezo makubwa Mkuu wa mkoa huyo ameyakagua magari hayo na atakabidhiwa magari 18 ambayo yamekamilika.
POL3
Baadhi ya magari ambayo tayari yamekamilika kwa matengenezo.
………………………………………………………………………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda Septemba 15, 2017 ametembelea na kukagua ukarabati mkubwa wa magari 26 ya polisi yaliyopelekwa mkoani Kilimanjaro yakiwa mabovu ili yafanyiwe ukarabati na kubadilishwa muundo wake na kuwa maalum kwa kazi za kipolisi.
Mhe. Makonda ameambiwa tayari magari 18 yamekamilika
kwa kufungwa vifaa mbalimbali ikiwemo matairi mapya, taa,vioo, kunyooshwa bodi na kupakwa rangi ikiwa ni pamoja na kuandikwa maandishi ya polisi.
Mhe. Makonda amesema ameridhishwa na kazi iliyofanyika na kwamba  atakabidhiwa magari hayo mwanzoni mwa mwezi Oktoba
Amesema Magari hayo yenye mwonekano kama yale ya UN yatakuwa na uwezo wa kubeba Askari tisa nyuma wakiwa wamekaa ambapo askari watatu watakuwa wakitazama nyuma, watatu kushoto, watatu kulia na mmoja mbele na wote wakiwa wamebeba silaha.
Aidha Makonda amesema kupatikana kwa magari hayo yatasaidia kupunguza vitendo vya Uhalifu kwa Wananchi.
RC Makonda amesema kuwa lengo lake ni kuona hakuna Mwananchi yoyote anaeibiwa au kuporwa kitu.
Hata hivyo amesema Baadhi ya Askari walikuwa wakipoteza maisha na kuporwa Silaha kutokana na aina ya Magari waliyokuwa wakitumia kutowapa uwezo wa kukabiliana na wahalifu hivyo Magari hayo yatamaliza matukio hayo.
Ameishukuru kampuni ya RSA Limited kwa kumuunga mkono kwa kujitolea kukarabati Magari 56 ya Jeshi la Polisi kwa kuyafanya kuwa ya kisasa na mapya.
Sanjari na hayo amesema Magari hayo yataenda kufanya Doria kwa masaa 24.
Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya RSA Bwana Manmohan Bhamra amesema kwa sasa Magari hayo ni sawa na Mapya kwakuwa yamewekwa vifaa vipya.
Amesema Magari yote watayakabidhi kwa wakati iliyakaongeze tija katika kuimarisha Ulinzi na Usalama kwa Wananchi.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger