TRA

TRA

Friday, September 1, 2017

SALA YA EID AL ADH'HA: MUFTI WA TANZANIA AWAASA WASILAMU KUITUNZA AMANI KWANI NI KAMA YAI

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
 

SHEIKH Mkuu wa Tanzania, Mjufti Abubakary Bin Zubeiry, amewaasa Waislamu nchini kuitunza amani kwani ni kama yai.
"Unajua yai lilivyo, ukilichezea likakuponyoka na kudondoka chini, huwezi tena kulikusanya na kulitumia, hivyo niwajibu wetu sisi Waislamu na wananchi kwa ujumla kuitunza amani tuliyo nayo na huu ndio ujumbe wangu muhimu kwa leo hii." Alifafanua Mufti Zubeiry baada ya ibada ya sala ya Eid Al Edh'ha na Baraza la Eid lililofanyika Masjid (Msikiti) wa Taqwa, ulioko Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam leo asubuhi Septemba 1, 2017.
Mufti Zubeiry amesema, Mwenyezimungu aliwaambia waliofarakana kuwa hawawezi kuingia peponi mpaka wakapatane kwanza, na kwa hakika tunawaomba watu wote waliohitilafiana, wenye chuki, wenye vinyongo, wenye vifundo, waondoshe na leo ndio siku ya kukaa pamoja na kula pamoja, katika sikukuu hii ya Eid al hadh'ha, alisema Mufti.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger