Waziri Mkuu ,Mh.Kassim Majaliwa akikabidhi cheti kwa Mwakilishi wa TBL Group, Emmanuel Christopher (kushoto),kutokana na mchango unaotolewa na kampuni kukuza elimu ya ufundi nchini,(katikati ) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama
Mariam Zayumba mmoja wa wahitimu kupitia program hiyo akichapa kazi katika kiwanda cha TBL Mwanza
Kulwa Kwangu mmoja wa wahitimu wa programu hiyo akiwa mitamboni katika kiwanda cha TBL
…………………..
KAMPUNI ya TBL Group imeeleza kuwa itaendelea kuunga mkono jitihaza za serikali kupunguza ajira nchini kwa
kuwawezesha vijana wa kitanzania kupata elimu ya ufundi stadi katika
vyuo vya VETA kupitia mpango maalumu wa kupata elimu zaidi ya vitendo
kuliko nadharia unaojulikana kitaalamu kama Dual Apprenticeship
programme
Akihojiwa
mjini Dodoma muda mfupi baada ya kupokea cheti cha kutambua mchango wa
kampuni kuendeleza vijana kupitia elimu ya ufundi wakati wa hafla ya uzinduzi wa miongozo ya Kitaifa ya Kusimamia Mafunzo ya Vitendo kwa Wahitimu
(Internship Guidelines) na Mafunzo ya Uanagenzi (Apprenticeship
Guidelines) mahala pa kazi,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Kassim Majaliwa,Mwakilishi wa TBL
Group,Emmanuel Christopher,alisema kampuni inaamini kuwa mpango wa
kuwapatia vijana elimu ya ufundi utawezesha kupunguza tatizo la ajira
nchini na ndio maana ni mdau wake.
Alisema vijana waliofadhiliwa
na kampuni hiyo na kupatiwa mafunzo katika fani ya umeme wa viwandani
kupitia program hiyo wameweza kupata maarifa makubwa ya kazi kwa vitendo
kwenye kiwanda cha TBL cha Ilala ambapo baada ya kuhitimu masomo wameweza kuajiriwa na wanaendelea kufanya vizuri.
“Mpango
huu utasaidia kuodoa tatizo la ajira nchini hususani katika kipindi
hiki tunapoelekea kwenye uchumi wa viwanda kwa kuwa viwanda ni moja ya
sekta yenye nafasi nyingi za ajira na vinahitaji wataalamu wa fani
mbalimbali hususani zile za ufundi”.Alisema Christopher.
Wakati
wa kuzindua miongozo hiyo,Waziri Mkuu,Mh.Kassim Majaliwa alisema
itasaidia kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kuhakikisha Taifa
linakuwa na nguvu kazi yenye weledi wa kutosheleza mahitaji ya soko la
ajira na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
SHARE
No comments:
Post a Comment