Mabingwa watetezi wa Kombe la
Shirikisho barani Afrika timu ya TP Mazembe imetinga hatua ya nusu
Fainali kwa kushindo ya Michuano ya Shirikisho baada ya kuwatandika
Waarabu wa Sudan,Al-Hilal Obeid kwa mabao 5-0 na kuwatupa nje kwa jumla
ya magoli 7-1.
TP Mazembe wakiwa kwenye dimba lao
la Stade Fredric Kibassa Maliba lilipo Mjini Lubumbashi waliingia
uwanjani wakiwa na ushindi magoli 2-1 ambao waliupata Sudan wiki
iliyopita.
Alikuwa beki kisiki wa Mazembe
Jean Kassusla aliwanyanyua mashabiki waliokuwa wamejaa kwa kuishangilia
timu yao dakika ya 39 akifunga bao kwa mkwaju Mkali wa Mita 18 na
kumshinda Mlinda mlango wa Al-Hilal hadi mapumziko Wenyeji walikuwa
mbele kwa bao 1-0.
Jean Kassusla akipiga Mpira wa adhabu ulioenda moja kwa moja hadi golini.
Kipindi cha pili kilikuwa kigumu
kwa Wasudan hao kwani waliweza kutandikwa bao nne huku wakizidiwa kila
idara na Mazembe wakicheza kwa kushambulia lango kama nyuki dakika ya 49
Mshambuliaji raia Wa Mali,Adama Traore alifunga bao la pili na dakika
tano Ben Malango alipigilia Msumari wa tatu.
Akitokea benchi Mshambuliaji wa
Congo,Elia Meshak aliifungia Mazembe bao la nne kwa kuwachambua mabeki
wa Al-Hilal kabla ya kuachia shuti kali huku wakiwa wanajiuliza beki
kisiki Issam Mpeko aliupigilia chuma cha tano na kuweza kuwanyamazisha
Waarabu hao na kutupwa nje ya hatua ya nane bora.
Kwa Matokeo hayo TP Mazembe
wametinga hatua ya Nusu Fainali la Shirikisho barani Afrika huku
wakisaka nafasi ya kuchukuwa kombe hilo kwa mara ya pili Mfululizo
ikumbukwe hao ndo mabingwa watetezi na watakutana na timu ya FUS Rabat
ya Morocco ambao nao walitinga Nusu baada ya kuwachapa Watunisia timu ya
CS Sfaxien kwa jumla ya mikwaju 4-3 ya Penalti.
SHARE
No comments:
Post a Comment