Muda mfupi baada ya kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga kutangaza
kutoshiriki katika marudio ya Uchaguzi Mkuu mpaka Tume ya Uchaguzi
ifanyiwe mabadiliko, Tume hiyo imetangaza kundi la watu sita ambalo
litasimamia uchaguzi huo.
Walioteuliwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Ezra Chiloba, Naibu wake
Betty Nyabuto, Mkurugenzi wa Usajili wa wapiga kura pamoja na Mkuu wa
Operesheni za Uchaguzi Immaculate Kasait, Naibu wake Mwaura Kamwati,
Mkuu wa Operesheni za Tume na Mkuu wa Teknolojia James Muhati.
Uchaguzi wa marudio Kenya umepangwa kufanyika Oktoba 17, 2017 kutokana
na ruhusa ya Mahakama ya Juu nchini humo kufuatia kesi ya kupinga
matokeo iliyofunguliwa na Odinga.
SHARE
No comments:
Post a Comment