WAKALA WA VIPIMO (WMA)
SIKU YA VIPIMO DUNIANI
VIPIMO VINAVYOTUMIKA KATIKA SEKTA YA
USAFIRISHAJI
(MEASUREMENT
FOR TRANSPORT)
Mei,
20 kila mwaka nchi nyingi duniani husherehekea siku ya vipimo duniani. Mwaka huu kauli mbiu ( theme)
ya maadhimisho ni vipimo katika sekta ya usafirishaji (measurement for transport) .
Shirika
la Vipimo Duniani (OIML) hutoa mapendekezo
na miongozo ya kimataifa katika nchi mbalimbali mojawapo ikiwa ni
Tanzania kupitia Wakala wa Vipimo kuhusiana na matumizi ya vipimo sahihi katika biashara, na sasa tuko kwenye mpango wa
kuingia katika sekta za afya, usalama na
mazingira, nia na lengo likiwa ni kuleta usahihi katika dhana nzima ya vipimo
kwa dunia nzima.
Hivyo,
katika Sekta ya Usafirishaji kwa mfano ambayo ndio theme ya Siku ya Vipimo Duniani; Mizani itumikayo barabarani, au kwenye viwanja vya ndege au
katika vituo vya mabasi ni lazima
ihakikiwe na kuthibitishwa na Wakala wa
Vipimo ili kupata usahihi wakati wa kupima uzito wa magari au
mizigo mbalimbali. Kama Mizani hiyo haitathibitiwa basi usalama wa wasafiri
pamoja na mizigo yao utakuwa mashakani.
Vile vile, Vyombo vingi vya usafiri ili viweze kusafiri kutoka sehemu moja
kwenda nyingine huhitaji nguvu yaani mafuta au gesi. Mafuta au gesi hutolewa
kwa vipimo sahihi ili kuhakikisha chombo kinafika sehemu sahihi kulingana na
kiasi cha mafuta/gesi iliyochukuliwa kituoni. Vipimo ambavyo vyombo vya usafiri
(Ndege, Mabasi, Magari) huchukuwa mafuta/gesi ni Vituo vya mafuta (Dispensing
pumps) na Flow meters.
Kupitia
Maadhimisho haya tutaeleza majukumu ya Wakala wa Vipimo kwa ujumla na
kubainisha umuhimu wa usahihi wa Vipimo nchini. Vile vile tutajikita zaidi
katika sekta ya usafirishaji ambayo ndio kauli mbiu ya maadhimisho.
JUKUMU LA WAKALA WA VIPIMO TANZANIA
·
Wakala wa Vipimo inalo jukumu la kumlinda mlaji na umma kwa ujumla
kupitia uhakiki na uthibiti wa vipimo vinavyotumika katika biashara na huduma
nyingine, kuhakikisha kuwa vipimo hivyo ni sahihi na vinatumika kwa usahihi
kulingana na Sheria ya Vipimo Sura 340 mapitio ya mwaka 2002 na maboresho yake
ya mwaka 2016 pamoja na kanuni zake.
·
Hivyo, Jukumu kuu la
Wakala wa Vipimo ni kumlinda mlaji kupitia matumizi ya vipimo sahihi.
KAZI ZA WAKALA
· Kuilinda jamii kutokana na madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya vipimo katika Sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira.
·
Kudhibiti ufungashaji wa bidhaa (Net quantity & lebelling)
·
Kuwa kiungo cha Taifa letu na taasisi
za Kikanda na Kimataifa katika masuala ya vipimo (legal Metrology)
·
Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu
masuala ya vipimo kwa wadau
·
Kuhakikisha vifaa vyote vitumikavyo
nchini vinakuwa na ulinganisho sahihi na ule wa Kimataifa.
KAZI
ZA WAKALA WA VIPIMO KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI
Kuhakiki mizani mikubwa
inayotumika barabarani (Weighbridges/Axle
Weighers). Weighbridges ni mizani
zinazofungwa barabarani kwa ajili ya kupima uzito wa magari makubwa. Mizani
hizi hutumika kupimia magari ya kubebea mizigo/mabasi. Hufungwa barabarani kwa lengo la kupima uzito wa magari ili yasiharibu
miundombinu ya barabara yasisababishe ajali.
Kuhakiki mizani aina ya Platform, Counter Scales & Spring
Balances Mizani hii mara nyingi hutumika Airport, bandarini,
Posta na katika vituo vya mabasi kwa ajili
ya kupimia uzito wa mizigo inayosafirishwa katika sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Vile vile Mizani hii hutumika Posta kwa ajili ya kupimia vifurushi mbalimbali
vinavyosafirishwa toka eneo moja kwenda eneo
jingine. Vifurushi hivyo hutozwa gharama za kusafirishia kulingana na
uzito wake. Mizani zote hizi yote upima uzito wa mizigo mbalimbali.
Kwa kutumia vipimo hivi,
wamiliki wa mizigo au wa vyombo vya usafiri hutozwa nauli za mizigo hiyo kulingana
na uzito wa mizigo husika. Pia, kutumia mizani katika vituo vya usafirishaji
hupunguza uwezekano wa kuzidisha uzito na kuepusha ajali za barabarani zinazotokana
na kuzidisha uzito.
Katika vituo vya mafuta na
bandarini kuna Dispensing pumps na Flow meters, hivi ni Vipimo ambavyo
vyombo vya usafiri kama Ndege, Mabasi, Magari huchukuwa mafuta/gesi. Mafuta au
gesi hutolewa kwa vipimo sahihi ili kuhakikisha chombo kinafika sehemu sahihi
kulingana na kiasi cha mafuta/gesi iliyochukuliwa kituoni.
FAIDA ZA KUTUMIA VIPIMO KATIKA SEKTA YA
USAFIRISHAJI
A:
Kuna faida mbalimbali zinazopatikana kwa kutumia vipimo vya uzito katika sekta
ya usafirishaji, baadhi ya faida hizo ni pamoja na:-
i) Kulinda miundombinu ya barabara kupitia mizani
(Weighbridges) zinazofungwa barabarani.
ii) Husaidia kupunguza ajali barabarani kwa magari yanayobeba
mizigo.
iii) Husaidia wateja kutozwa ada ya mizigo/vifurushi vinavyosafirishwa
kulingana na uzito wa mzigo.
B: Vipimo vya kupimia mafuta na gesi (Volume Measurements)
Vyombo vingi vya usafiri ili viweze kusafiri kutoka
sehemu moja kwenda nyingine huhitaji nguvu yaani mafuta au gesi. Mafuta au gesi
hutolewa kwa vipimo sahihi ili kuhakikisha chombo kinafika sehemu sahihi
kulingana na kiasi cha mafuta/gesi iliyochukuliwa kituoni. Vipimo ambavyo
vyombo vya usafiri (Ndege, Mabasi, Magari) huchukuwa mafuta/gesi ni Vituo vya
mafuta (Dispensing pumps) na Flow meters.
Jaribu
kufikiri kwa mfano ndege inaondoka ikiwa imepakia abiria pamoja na mizigo na
imejaza mafuta yakiwa pungufu yaani haijazingatia matumizi sahihi ya vipimo ni
dhahiri itakapokuwa angani itaishiwa mafuta, hivyo usalama wake na wa abiria
utakuwa mashakani. Hivyo, Vipimo vina umuhimu mkubwa sana katika sekta ya
usafiri.
C. Kipimo cha kupima mwendokasi (Speed Measuring Device)
Speed measuring device ni kifaa kinachotumika na Traffic kupima speed (Mwendo kasi)
wa magari yanayo tembea barabarani. Kifaa hicho hupima na kurekodi mwendokasi
wa gari linalokimbia barabarani. Faida ya kutumia vifaa hivi vya kudhibiti
mwendokasi ni dhahiri, mojawapo ikiwa ni kudhibiti ajali barabarani.
D.
Vipimo vingine katika sekta ya usafiri ambavyo Wakala wa Vipimo ipo kwenye
mchakato wa kuvihakiki ni taximeter pamoja na tyre
pressure gauge.
CHANGAMOTO
i.
Upungufu wa watumishi na vitendea
kazi katika kufanya shughuli za vipimo.
ii.
Uelewa mdogo wa sheria za vipimo kwa
jamii ya wafanyabiashara na wananchi.
iii.
Kuwepo kwa mizani mingi batili na
isiyokuwa na ubora sahihi inayoingizwa nchini kinyemela na baadhi ya
wafanyabiashara wasio waaminifu. Changamoto hii inasababishwa na uhaba wa
mizani nchini na hata ile michache inayopatikana/ kuagizwa toka nje ni ghali kwa wananchi wa kawaida kumudu.
iv.
Uhaba wa Vipimo (hasa mizani) halali nchini.
Hivyo
tukiwa tunaadhimisha Siku ya Vipimo Duniani ambayo mwaka huu imejikita katika
Sekta ya Usafirishaji, ni vyema tukatambua kuwa umuhimu wa Vipimo sahihi uko katika kila sekta ya maisha
yetu hapa nchini. Baadhi ya sekta hizo ni kama Biashara, Afya, Usalama,
Mazingira na nyingine nyingi. Ni wajibu wetu pia kutambua kuwa Wakala wa Vipimo
ndio iliyopewa majukumu haya muhimu ya kumlinda mwananchi katika harakati zake
za kujenga uchumi.
Baadhi ya maofisa vipimo (Picha kwa Hisani ya Wakala wa Vipimo nchini.)
SHARE
No comments:
Post a Comment