Mratibu wa Jumuiya ya kumuendeleza
mtoto wa kike kielimu (FAWE) Hinda Abdalla Ajmy akizungumza na walimu
na wanafunzi walioshiriki mafunzo ya siku tano ya Ufundi na Hisabati
katika Hoteli ya Afrika House Shangani, Mjini Zanzibar.
Mhandisi wa ujenzi Talha Masoud
akiwaonesha washiriki wa mafunzo hayo michoro ya majengo aliyobuni na
kuwataka wanafunzi wa kike kujitokeza kujiunga na fani hiyo kwani
inasoko kubwa hivi sasa.
Mtaalamu wa Teknolojia ya
Mawasiliano ya Habari (ICT) Raya Said Khalifa akiwasisitiza wanafunzi wa
kike kujiunga na fani hiyo ili kwenda na wakati wa sasa wa sayansi na
teknolojia.
Wanafunzi wa skuli ya wanawake
Tumekuja wakifanya majaribio ya huduma ya kwanza katika mafunzo ya siku
tano ya sayansi yaliyofanyika Hoteli ya Africa House Shangani Zanzibar.
Walimu wa skuli walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia majaribio ya kisayansi yaliyokuwa yakifanywa na washiriki wenzao.
Mgeni rasmi Afuwa Mohammed
akiyafunga mafunzo ya siku tano kuhusu masomo ya sayansi yatokanayo na
enginiaring na hisabati mara tuu baada ya kuwahutubia.
(PICHA NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR.)
SHARE
No comments:
Post a Comment