|
Dar
es Salaam, TANZANIA. Tarehe 21 Septemba 2017, Kaimu Balozi wa Marekani nchini
Tanzania Dk. Inmi Patterson aliwaapisha wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps
wapatao 57 kuhudumu nchini Tanzania katika kipindi cha miaka miwili katika
hafla iliyofanyika katika ofisi za Peace Corps jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi hawa wa kujitolea wa Kimarekani watakaofanya kazi katika sekta ya
elimu watapangiwa kuhudumu katika wilaya za Iringa, Mufindi, Same, Kyela,
Masasi, Maswa, Singida Vijijini, Lushoto, Chamwino, Hai, Rombo, Wete, Rungwe,
Njombe, Iringa Vijijini, Sumbawanga, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Hanang,
Mbeya, Nachingwea, Hanang, Iramba, Kiomboi, Mbeya Rural, Shinyanga na Singida
Mjini.
Mgeni rasmi katika hafla hii alikuwa ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Leonard D. Akwilapo.
Hafla hii
ilihudhuriwa pia na wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps wanaoendelea
kuhudumu na wale waliohudumu hapo zamani pamoja na maafisa kutoka mashirika
mengine yanayojihusisha na wafanyakazi wa kujitolea.
Akizungumza na wafanyakazi
hao wa kujitolea Kaimu Balozi Patterson alisema:
"Wakati ambapo kuna
uwezekano kwamba mnaweza kuwa Wamarekani wa kwanza kuishi na wafanyakazi
wenzenu au majirani wa Kitanzania, ni wazi kwamba kwa Watanzania hao nyinyi
mtaendelea kuwa wawakilishi wa Watu wa Marekani."
Peace Corps ni taasisi ya
Serikali ya Marekani iliyoanzishwa na Rais John F. Kennedy mwaka 1961 ambayo
hivi sasa inahudumia zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea zaidi ya 7,000 katika
zaidi ya nchi 70 duniani. Kwa zaidi ya miaka 50, Peace Corps imekuwa taasisi
inayoendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi na kitamaduni zisizoegemea
mrengo wowote wa kisiasa na kidini. Peace Corps ina dhamira ya kukuza amani na
urafiki duniani kwa kutekeleza malengo matatu yafuatayo:
- Kutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani watakaochangia kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi itakayohitaji wafanyakazi hao;
- Kukuza uelewa kuhusu Wamarekani miongoni mwa watu katika jamii zinazohudumiwa na Wafanyakazi wa kujitolea;
- Kuimarisha uelewa wa Wamarekani kuhusu dunia na watu wake.
Zaidi
ya wafanyakazi wa kujitolewa wa Peace Corps 2,500 wamehudumu nchini Tanzania toka
mwaka 1961. Peace Corps hutoa
wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wenye utaalamu katika nyanja mbalimbali
ambao hupangiwa kufanyakazi katika jamii wakifundisha katika shule za sekondari
(hisabati, sayansi na Kiingereza), wakitoa elimu ya afya na utunzaji wa
mazingira.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari
ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa simu namba: +255 22 229-4000 au kwa
barua pepe: DPO@state.gov.
SHARE
No comments:
Post a Comment