TRA

TRA

Friday, September 22, 2017

Halotel, USCAF kufikisha Mawasiliano vijiji vipya zaidi ya 100

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

 

Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Halotel kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (USCAF), wamekubaliana kufikisha huduma ya mawasiliano kwa vijiji vipya zaidi ya 100 vilivyoko katika maeneo ya mipakani na pembezoni mwa nchi baada ya kuingia makubaliano yatakayo iwezesha kampuni hiyo ya simu kujenga minara mipya arobaini na saba (47) katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu ya adhma ya serikali ya kufikisha huduma za mawasiliano maeneo ya vijijini.


Akizungumza juu ya Makubaliano hayo wakati wa uzinduzi wa moja ya Minara iliyojengwa kwa ushirikiano kati ya Kampuni hiyo na Mfuko wa Maendeleo kwa wote, (USCAF) Uliofanywa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Wilayani Gairo, Mkoani Morogoro, pamoja na Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma, Naibu Mkurugenzi wa Ufundi na Uhandisi wa Halotel Bwana, Trieu Thanh Binh, Amesema Kampuni hiyo itahakikisha inazingatia makubaliano iliyoingia baina yake na serikali ili kuhakikisha wanatimiza adhama ya serikali ya kufikisha huduma ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini huku akibainisha kuwa tayari wameanza utekelezaji wa makubaliano hayo.


“Katika makubaliano tuliyoingia na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, tutafikisha huduma ya mawasiliano katika vijiji vipya zaidi ya mia moja 100 na pia tumekubaliana kulenga maeneo ya vijijini ambayo yako katika mipaka ya nchi na maeneo mengine ambayo yako maeneo yasiyo fikika kwa urahisi. Maeneo yote ambayobado hayajafikiwa na huduma za Mawasiliano kabisa hivyo tutahakikisha tunafikisha huduma hiyo kwa wakati ili kuendana na kasi ya Serikali katika kutekeleza vipaumbele vyake,” Alisema Binh na kuongeza.


“Ni lengo letu kuhakikisha tunafikisha huduma bora za Mawasiliano na sio bora mawasiliano katika maeneo yote ambayo yameainishwa, tuna malengo ya kuhakikisha tunafikia maeneo yote ya nchi na kutimiza Malengo ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, tutahakikisha tunazingatia makubaliano baina yetu na mfuko.



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (Katikati) akitoa Maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Ufundi na Uhandisi wa Halotel, Trieu Thanh Binh pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF) Mhandisi, Peter Ulanga wakati wa Uzinduzi na ukaguzi wa moja ya Minara iliyojengwa kwa Ushirikiano wa Halotel na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF), iliyojengwa katika kijiji cha Haneti, wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma. 

Binh, Ametaja baadhi ya Maeneo ambayo yatafikiwa na huduma za Mawasiliano katika mabubaliano hayo kuwa ni pamoja na Endamalek na Mbulumbulu vilivyoko Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha, Vijiji vingine ni Iyogelo, Kasubuya, Nyalubele, Nyaluguguna, Nyinjudu vyote vya Wilayani Nyangwale Mkoani Geita, Vijiji vingine vilivyo bainishwa ni Chanjale, Ngujini, na Songoa vilivyoko wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro huku vijiji vya Kilimanihewa, Mazoezi, Mtepeche, Nampemba vya Wilaya ya nachingwea Lindi pamoja na Chauru, Mhata, Mirewe na Nambombwe navyo vikifikiwa na huduma hizo za Mawasiliano.


Vijiji vingine ambavyo pia viko katika mradi huo ni pamoja na Kikaro, Kweikonje, Masimbani, Mihunga na Miono vya Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, huku vijini vilivyoka katika kata za, Kilondo, Lumbila, Lupingu vya Wilaya ya Ludewa pamoja na Ipelele na Lupila vya Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe nazo zikifikiwa na huduma hizo pamoja na vijiji vingine vingi ambavyo havitajwa katika orodha hiyo.


Hivi karibuni, Akizungumza baada ya kuzindua moja ya Mnara uliojengwa kwa Ushirikiano kati ya Kampuni hiyo na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF) Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa. Makame Mbarawa ametoa wito kwa kampuni hiyo kuhakikisha inakamilisha mradi huo kwa wakati na kusisitiza kuwa Serikali itasimamia na kutoa Mazingira rafiki kwa kampuni zote za Mawasiliano zilizoingia katika makubaliano na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote na kusisitiza kuwa ni vyema pia wananchi wakazingatia matumizi bora na salama ya huduma za mawasiliano na simu kwa kuzingatia sharia na taratibu zilizowekwa na Mamlaka husika.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger