Makandege alidai hayo jana mbele ya
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na kueleza mahakama kuwa mshitakiwa huyo
alifanyiwa upasuaji na kuwekwa puto tumboni.
Alidai kuwa katika mashauri
yaliyopita, mahakama ilitoa amri mara mbili, zote zikielekeza mshitakiwa huyo
apelekwe Hospitali ya Muhimbili lakini haijatekelezwa.
Aliomba mahakama izingatie ugonjwa
wa mshitakiwa na iamuru apelekwe moja kwa moja Muhimbili kwani ndio
hospitali ya juu ya serikali nchini ambayo inategemea kuwa na
wataalamu na vifaa stahiki vya ugonjwa unaomkabili.
"Upande wa jamhuri unatambua haya
lakini kwa ridhaa yao wao wamempeleka mshitakiwa Amana hospitali. Swali ambalo
mahakama isaidie kujibu pamoja na jamhuri, ni je, kumpeleka mshitakiwa wa
kwanza hospitali ya Amana, magereza na jamhuri wameshindwa kutii amri ya
mahakama?," alihoji Makandege.
“Mahakama haikumungunya maneno katika
kutoa amri yake, ambapo ilitamka kwenye amri hiyo kwamba mshitakiwa huyo
apelekwe katika hosipitali ya taifa ya Muhimbili, wao kumpeleka Amana
wametekeleza amri gani?” Makandege aliendelea kueleza.
Alidai amri ya mahakama
haijatekelezwa hivyo upande wa mashitaka umekaidi amri hiyo.
"Mahakama ndio mahala amri zote
zitaheshimiwa kwa pande zote mbili kwa kuwa nchi inafuata demokrasia na utawala
wa sheria," alidai Makandege.
Makandege alidai kuwa kilichofanyika ni
kinyume na amri ya mahakama na kinyume na sheria za magereza kifungu cha 53 (1) ambacho
kinatoa fursa kwa mtu yoyote aliyeko gerezani kama anaumwa kufikishwa hospital
ili apate matibabu.
Alidai kuwa ni rai yake kuwa mahakama
haina uwezo wa kusikiliza shauri husika lakini inamamlaka ya kuhakikisha
tararibu za mahakama zinafuatwa na kuhakikisha haki inatendeka.
Wakili wa Serikali, Vitalis Peter
alidai hakuna amri yoyote ya mahakama ambayo jamhuri
haijaitekeleza.
Alidai kuwa ni kweli kifungu cha 53 (1)
cha sheria ya magereza kinaipa mamlaka magereza kumpeleka mtuhumiwa hospitali
kama anaumwa na kwamba magereza wana wataalamu wao na hospitali yao na ndio
wanakaa na mtuhumiwa na wanamuangalia kwa mara ya kwanza, wakishindwa kumtibu
ndio wanampa rufaa.
Wakili Peter alidai kuwa
mshitakiwa alihudumiwa na wataalamu wa magereza na kumpeleka hospitali ya juu
yao ambayo ni Amana, baada ya Amana alipatiwa matibabu na daktari bingwa
kutoka muhimbili Dk Wilson Mgamba ambaye alimuona mtuhumiwa na kujiridhisha na
afya yake.
"Wakili awasiliane na mteja wake
kwanza kwasababu kashapatiwa matibabu na magereza hawachaguliwi kumpeleka mtu
hospitali ambao ndio wanaweza kujua ugonjwa alionao na wapi pa
kumpeleka," alidai Vitalis.
Baada ya kuwasilisha hayo, Wakili Makagande
alidai kuwa haiwezekani daktari kuchukua vifaa vyote kuvipeleka katika magereza
ya Segerea na kwamba mteja wake hajapatiwa matibabu hayo na yuko mahakamani
anaweza kuongea mwenyewe.
Wakili Makandege alieleza mahakama
kwamba kauli ya wakili wa serikali kudai kwamba Magereza hawapangiwi sehemu ya
kumpeleka mtuhumiwa au mfungwa ambaye yupo mikononi mwao kwa matibabu, ni
dharau kwa amri na heshima ya mahakama.
Pia aliongeza kuwa taratibu za ndani
zilizowekwa na Magereza haiwezi ikawa juu ya amri za mahakama na sheria za
nchi. “Uwepo kwa taratibu za magereza haiwezi ikaifanya amri za mahakama
kusiginwa. Taratibu za ndani za magereza haiwezi ikawa juu ya amri za mahakama.
Kauli hiyo ya wakili msomi mwandamizi wa serikali inaonyesha ni jinsi gani
magereza wameidharau mahakama yako tukufu,” aliongeza Makandege.
Hata hivyo, Hakimu Shaidi alisisitiza
mshitakiwa huyo apelekwe katika hospitali ya Muhimbili kama ilivyotoa maagizo
awali.
Kwa upande wake, James Rugemarila
aliiomba mahakama, magereza waweze kumruhusu kuonana na mawakili wake
kwasababu anambambo mengi ya kuongea nao.
Alidai kuwa anamawakili 10 na
kunawakati anahitaji kuongea nao lakini anauwezo wa kuwaona wawili tu hivyo
anaomba aweze kupatiwa dakika 30 kuzungumza nao kabla hajarudishwa mahabusu.
Seth na Rugemarila wanakabiliwa
na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha
mtandao wa uhalifu , kighushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha
kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kuisababisha hasara
ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
SHARE








No comments:
Post a Comment