Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima
ya (NHIF) Afya Ofisi ya Mbeya, Isaya Shekifu akizungumza katika
Viwanja vya Tandale Wilayani Rungwe ambapo Tamasha la Ngoma za asili
linalojulikana kwa Tulia Traditional Dances Festival 2017
Watu mbalimbali wakipima afya katika tamasha hilo.
B. Angella Mziray Meneja wa
Masoko Mfuko wa Taifa wa Bima ya (NHIF) akizungumza na kuelezea huduma
mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo katika tamasha hilo.
Mmoja wa wazee wakipata ushauri wa kiafya kutoka kwa ofisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya (NHIF).
Wananchi mbalimbali waliojitokeza
kupima afya zao na kupata ushauri wakipata huduma mbalimbali katika
banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya (NHIF)
Naibu Spika Dk. Tulia Ackson
akizungumza katika tamasha la Tamasha la Ngoma za asili linalojulikana
kama Tulia Traditional Dances Festival 2017 Tamasha hilo linafanyika
kwenye Viwanja vya Tandale Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
…………………………………………………………………..
WATU zaidi ya 800 wamejitokeza
kupima afya ya magonjwa yasiyoambukiza katika Viwanja vya Tandale
Wilayani Rungwe ambapo Tamasha la Ngoma za asili linalojulikana kwa
Tulia Traditional Dances Festival 2017 lililoandaliwa na Naibu Spika Dk.
Tulia Ackson linafanyika.
Akizungumzia hili, Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya (NHIF) Afya Ofisi ya Mbeya, Isaya Shekifu alisema pamoja na kuenzi utamaduni wamegundua kuwa watu wengi hawana utamaduni wa kufika Hospitalini kwa ajili ya kupima afya zao kwa ajili ya kupata ushari na tiba ya magonjwa yasioambukiza ambayo ni tishio kubwa kwa afya za wengi.
Alisema Mfuko uliona utumie fursa ya mashindano ya Ngoma za asili kwa ajili ya kuwafikia watu wengi ili waweze kupima na kupatiwa ushauri na elimu juu ya magonjwa mbalimbali ikiwemo Sukari, shinikizo la damu na unene ulipitiliza.
Akizungumzia hili, Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya (NHIF) Afya Ofisi ya Mbeya, Isaya Shekifu alisema pamoja na kuenzi utamaduni wamegundua kuwa watu wengi hawana utamaduni wa kufika Hospitalini kwa ajili ya kupima afya zao kwa ajili ya kupata ushari na tiba ya magonjwa yasioambukiza ambayo ni tishio kubwa kwa afya za wengi.
Alisema Mfuko uliona utumie fursa ya mashindano ya Ngoma za asili kwa ajili ya kuwafikia watu wengi ili waweze kupima na kupatiwa ushauri na elimu juu ya magonjwa mbalimbali ikiwemo Sukari, shinikizo la damu na unene ulipitiliza.
Alisema wananchi wengi wamehamasika na kujitokeza kupima na kupata ushauri kutoka kwa madaktari waliopo katika viwanja hivyo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Bi. Anjela Mziray alisema pamoja na kupima
afya katika mashindano hayo ambayo huduma hutolewa bure pia Mfuko
unahamasisha na kusajili watoto wa chini ya umri wa miaka 18 na huduma
ya bima ya afya. Huduma hii inajulikana kwa jina la Toto Afya Kadi.
Alisema zoezi la kuandikisha
linafanyika kiwanjani hapo na kadi kutolewa ndani ya muda mfupi kwa
mchango wa shilingi 50,400 tu kwa mwaka kwa kila mtoto ambapo mtoto
atapata matibabu kwa mwaka mzima katika Zahanati,Vituo vya Afya na
Hospitali zote zilizosajiliwa na Mfuko huo Tanzania nzima.
Aidha alitoa wito kwa wazazi na
Walimu kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwa shule nyingi za bweni
zinakabiliwa na changamoto ya matibabu kwa wanafunzi hivyo kila
mwanafunzi akiwa na Bima ya afya itamrahishia kupata matibabu kwa
uhakika akiwa shuleni na hata wakati wa likizo.
Nao baadhi ya Wateja
waliojitokeza kupata huduma katika Banda la Bima ya Afya, Staford
Mwakasapa na Mwalimu Elizabeth Sekile ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama
cha Walimu Wilaya ya Rungwe wamepongeza utaratibu huo na kuongeza kuwa
huduma kama hiyo inapaswa kusambazwa katika kila mikusanyiko.
Walisema watu wengi hawana
utaratibu wa kwenda Hospitali kupima afya zao hadi waugue hivyo huduma
ya kutembelea na kutoa elimu napaswa kusogezwa na kuwa endelevu ili
kuokoa afya za wananchi.
Hata hivyo walitoa wito kwa
Serikali kuhakikisha wateja wenye kadi za matibabu ya Bima ya Afya
wanapata huduma zote zinazostahili ikiwemo upatikanaji wa Vifaa tiba
pamoja na madawa kwa wagonjwa
SHARE
No comments:
Post a Comment