Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za
Taifa-TANAPA, Bw. Allan Kijazi na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika
nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini
Makubaliano ya utekelezaji wa Mkataba wa Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda
wa Kusini mwa Tanzania utakao gharimu Shilingi bilioni 340 zilizotolewa kama
mkopo wenye masharti nafuu na Benki hiyo kwa Tanzania, Ofisi za Wizara ya Fedha
na Mipango, Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia nyuma ni Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha na Mipango Bw. Doto James, (wa pili kulia waliosimama akifuatiwa na
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi,
Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za
Taifa-TANAPA, Bw. Allan Kijazi na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika
nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini
Makubaliano ya utekelezaji wa Mkataba wa Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda
wa Kusini mwa Tanzania utakao gharimu Shilingi bilioni 340 zilizotolewa kama
mkopo wenye masharti nafuu na Benki hiyo kwa Tanzania
Benny
Mwaipaja, Dar es Salaam
BENKI
ya Dunia imeipatia Tanzania Mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani
milioni 150, sawa na takriban Shilingi bilioni 340 kwa ajili ya kutekeleza
mradi mkubwa wa kufungua fursa za utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania.
Mkataba
wa mkopo huo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha na Mipango, Bw. Doto James na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia
anayehudumia nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi, Bi. Bella Bird.
Bw.
James alisema kuwa mkopo huo umelenga kuimarisha miundombinu ya utalii katika
ukanda huo wa kusini ikiwemo ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, madaraja
pamoja na kuibua fursa nyingi za utalii ili kuvutia watalii wengi zaidi.
Alisema
pia kwamba mradi huo umelenga kuwajengea uwezo wananchi wanaozunguka maeneo ya
utalii kwa kuanzisha miradi itakayo chochea maendeleo yao ya kijamii na
kiuchumi pamoja na kuendeleza uhifadhi katika maeneo yao.
Aidha,
mkopo huo utatumika katika kampeni ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko
katika ukanda huo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania ili kuvutia watalii wengi
zaidi kutembelea maeneo hayo badala ya hali ilivyo sasa ambapo watalii wengi
wanatembelea vivutio vilivyoko ukanda wa Kaskazini.
Mradi
huo utakaotekelezwa kwa kiasi kikubwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa
Tanzania-TANAPA, utainufaisha zaidi Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mikumi, Udzungwa
na Pori la Akiba na Selous.
Alisema
kuwa manufaa hayo yatalenga kujengwa viwanja vya ndege, barabara hifadhini,
utunzaji wa mazingira utakao uwezesha mto Ruaha Mkuu kutiririsha maji muda wote
katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kupitia uwanda wa Usangu.
“Mpango
wa kuibua fursa za utalii katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania, umelenga
kuimarisha usafiri wa anga na nchi kavu ambapo uwanja mkubwa na wa kisasa
utajengwa mkoani Iringa pamoja na kuboresha barabara inayotoka Iringa hadi
Msembe yenye urefu wa kilometa 105” alisema Bw. James
Aisema
kuwa hatua hiyo inatarajia kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ya nchi na
kupunguza gharama za usafiri kutoka katika maeneo ya Zanzibar, Dar es Salaam na
Kilimanjaro hivyo kuongeza mapato ya Serikali.
Bw.
Doto James aliishukuru Benki ya Dunia kwa mkopo huo utakao changia kwa kiasi
kikubwa kukuza uchumi wa nchi na maendeleo ya wananchi wake kupitia sekta ya utalii.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali,
Gaudence Milanzi alisema kuwa mradi huo, utahusisha ujenzi wa viwanja 15 vya
ndege, ujenzi wa kilometa 982 za barabara kwenye hifadhi, kununua mitambo ya
kukarabati barabara, kuimarisha reli ya TAZARA ili kuwawezesha watalii kufika
kwenye Pori la Akiba la Selous.
Aidha,
alisema kuwa wananchi wanaozunguka eneo la mradi watapatiwa mafunzo ya namna ya
kuongoza watalii, kutoa huduma kwenye hoteli na kuwajengea uwezo wa kutengeneza
bidhaa zinazohusiana na utalii ili wajiongezee kipato.
Meja
Jenerali Milanzi alisema kuwa wanategemea mradi huo utaongeza idadi ya watalii
kutoka milioni moja hivi sasa hadi kufikia zaidi ya watalii milioni 2 ifikapo
mwaka 2020.
Akizunguza
wakati wa tukio hilo, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, hapa nchini Bi. Bella
Bird alisema kuwa mkopo huo ulioridhiwa na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo
Jijini Washington DC Septemba 28, 2017, umelenga kukuza uchumi wa Tanzania
kupitia sekta hiyo ya utalii na kupunguzia umasikini wananchi wake.
“Utalii
na uhifadhi vinakwenda pamoja na kwamba vitu hivyo viwili vitaisaidia nchi
kukua kiuchumi na kukuza ajira ya watu wake kwa kiwango kikubwa hivyo
kuondokana na umasikini ikichagizwa pia na kilimo” alisisitiza Bi. Bella Bird.
Alisema
sekta ya utalii inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ya watu
na wanyama, ujangili, na ndiyo maana Benki ya Dunia imeamua kuisaidia Serikali
na taasisi zinazojihusha na kudhibiti changamoto hiyo kwa kuzijengea uwezo wa
kukabiliana nazo.
Bi.
Bird alisema kuwa mradi huo utakuja na suluhisho la changamoto ya wananchi kuwa
sehemu ya uhifadhi kwa kuwapa miradi ya maendeleo itakayokuwa mbadala wa
shughuli walizokuwa wakifanya kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo kuanzisha utalii
wa kiutamaduni, kilimo ili waendeleze maisha yao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa
pili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania,
Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini Mkataba wa Mkopo
wenye masharti nafuu wa Sh. Dola za Marekani milioni 150 sawa na Shilingi
bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa
Tanzania, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.
Doto James (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za
Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi Bi. Bella Bird (kushoto) wakibadilishana Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu
wa Sh. bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii katika Ukanda
wa Kusini mwa Tanzania, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar
es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa
pili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania,
Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini Mkataba wa Mkopo
wenye masharti nafuu wa Sh. Dola za Marekani milioni 150 sawa na Shilingi
bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa
Tanzania, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.
Doto James (kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za
Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbiji Bi. Bella Bird, wakielekea kusaini
Mkataba wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa
ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es
Salaam
Baadhi ya Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, na
Katibu Mkuu Wizara ya maliaasili na Utalii( wa kwanza kushoto) wakifuatilia kwa
makini tukio la kusainiwa kwa Mkataba wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani
milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa
Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Ujumbe wa Benki ya Dunia walioshiriki tukio la Tanzania na Benki hiyo kutiliana saini mkataba wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam
SHARE
No comments:
Post a Comment