Rais wa Marekani
Donald Trump ametoa onyo kali kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong
un katika hotuba ndani ya bunge la Korea Kusini.
Bwana Trump alimzungumzia moja kwa moja rais Kim akisema kuwa ''silaha unazojilimbikia hazikufanyi wewe kuwa salama lakini zinakuweka katika hali hatari''.
Kiongozi huyo wa Marekani yuko katika ziara ya siku mbili nchini Korea Kusini katika ziara ya bara Asia.
Kwengineko katika hotuba yake amesema kuwa huku Korea Kaskazini ikiona uvumilivu kuwa udhaifu sasa kuna utawala mpya nchini Marekani.
- Marekani yatishia kuiadhibu Korea Kaskazini
- Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa
- Marekani: Korea Kaskazini haitutishi
Dunia haiwezi kuvumilia hatari inayosababishwa na taifa linaloongozwa na utawala usioaminika ambao unaitishia na silaha za kinyuklia.
Mataifa yote yaliowajibika yanafaa kuungana kuangamiza utawala wa kikatili wa Korea Kaskazini kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeuunga mkono, kupata usaidizi wowote ama hata kukubalika, alisema.
SHARE








No comments:
Post a Comment