TRA

TRA

Tuesday, November 7, 2017

KAMPUNI YA UDALALI YA MSAMA AUCTION MART YAENDELEA NA MSAKO WA CD FEKI JIJINI DAR ES SALAAM

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jana katika kituo cha Polisi Kanda Maalum Dar es salaam kabla ya kuanza kwa msako huo.
……………………………………………………………… Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi,
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo imeendelea na zoezi la ukamataji wa Wadurufu wa kazi za sanaa na
wakwepa kodi kupitia kazi hizo.
Zoezi hilo limeendelea katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam ambapo pia imesisitizwa kuendelea nchi nzima.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya kuanza kwa shughuli hiyo, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart amewaasa Wafanyabiashara wote kufuata taratibu kuhakikisha wanauza bidhaa zenye Stika ya TRA.
“Uzeni bidhaa  zenye Stika ya TRA, acheni kuwaibia Wasanii, wakati huu ni wakati wa Serikali kupata haki yake na Wasanii pia wapate haki zao,wafaidi jasho la kazi yao”, amesema Msama
Pia amewaasa Watanzania wanaonunua  kazi hizo za sanaa kuacha kununua kazi ambazo hazina Stika ya TRA,  amesema Watanzania wanapaswa kujifunza kulipa Kodi kupitia kazi hizo  zenye Stika halali ya TRA.
“Wale wanaoburn CD, Wanaoingiza nyimbo kutumia Kompyuta muache, zoezi hili sio Dar es Salaam pekee zoezi ni la nchi nzima na tutahakikisha kila anayenunua bidhaa hizo ananunua bidhaa zenye Stika”, amesisitiza Msama.
2 3
Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart na askari wakiwa  wamevamia moja ya duka linalofanya biashara ya kuuza kazi za Wasanii kwa
maeneo ya Kariakoo  jana jijini Dar.
4
Baadhi ya wauziaji wa CD hizo wamefuata utaratibu wa kuuza CD zenye Stika za TRA kama huyu muuzaji ambaye alikutwa akiuza CD zake zenye Stika eneo la Buguruni jana.
5
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Msama Auction Mart pamoja na polisi wakipita katika maduka mbalimbali eneo la Buguruni kukagua na kukamata CD ambazo hazina stika za TRA.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger