
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipokea Msaada wa Fedha Taslimu Sh. Milioni 5 kutoka kwa James Mlowe Meneja Mawasiliano na Masoko Mfuko wa Pensheni wa LAPF
kwa ajili ya kununulia mifuko 500 ya saruji katika kuchangia kampeni ya
ujenzi wa Ofisi za Kisasa za walimu katika shule za Msingi na Sekondari
Mko wa Dar es salaam.
Kampeni hiyo imeanzishwa na
Mkuu wa mkoa wa Mh.Paul Makonda katika jijini la Dar es salaam, ambapo
Ofisi zaidi ya 400 zitajengwa katika shule za jiji la Dar es salaam
hivyo kuboresha utendaji kazi wa waalimu hao, Kalia anayeshuhudia tukio
hilo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Kanali Charles Mbuge,
Makabidhiano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki ofisini kwa Mkuu wa
mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akimsikiliza Bw. James Mlowe Meneja
Mawasiliano na Masoko Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakati akizungumza
kabla ya kukabidhi msaada uliotolewa na LAPF kwa mkuu wa mkoa wa Dar
es salaam kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za walimu katika shule za
sekondari na Msingi katika mkoa wa Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mh. Paul Makonda akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika
Ofisini kwake katikati ni Bw. James Mlowe Meneja Mawasiliano na Masoko Mfuko wa Pensheni wa LAPF na kulia ni Kanali Charles Mbuge Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mh. Paul Makonda akisisitiza jambo wakati akizungumza katika
makabidhiano hayo yaliyofanyika Ofisini kwake lulia ni Bw. James Mlowe Meneja Mawasiliano na Masoko Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
SHARE








No comments:
Post a Comment