Mwanamfalme mmoja
nchini Saudi Arabia amefariki baada ya helikopta aliyokuwa akisafiria
kuanguka karibu na mpaka wa nchi hiyo na yemen, vyombo vya habari vya
serikali vimeripoti.
Chanzo cha ajali hiyo hakijabainika.
Saudi Arabia ilisema ilitungua kombora la masafa marefu lililokuwa limerushwa kutoka Yemen likiwa karibu na uwanja wa ndege wa Riyadh Jumamosi.
- Mwanamfalme akatwa shingo Saudi Arabia
- Wasaliti kunyongwa Saudi Arabia
- Wana wa ufalme wakamatwa Saudi Arabia
Taasisi hiyo ya kukabiliana na ufisadi iliundwa na mwanamfalme wa kwanza kwenye urithi Mohammed bin Salman.
Mwanamfalme Mansour bin Muqrin, aliyefariki, ni mwana wa mwanamfalme aliyekuwa wa kwanza katika urithi awali.
Babake, Muqrin bin Abdul Aziz, alitengwa na ndugu wa kambo wa Mfalme Salman miezi kadha baada yake kurithi ufalme mwaka 2015.
Shirika la habari la Okaz limesema taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema hakukuwa na manusura kwenye ajali hiyo ya ndege.
CHANZO: BBC
SHARE









No comments:
Post a Comment