Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk Albina Chuwa amesema
takwimu za Taifa lazima ziheshimiwe na si kila mtu anastahili kuzitoa.
Dk
Chuwa alisema hayo jana katika kipindi maalumu cha miaka miwili ya Rais
John Magufuli kilichorushwa na kituo cha televisheni cha Azam.
Alisema kazi ya kutangaza takwimu katika nchi zilizoendelea hufanywa na wataalamu na si kila mtu anapojisikia.
“Wenzetu
wa Marekani, si rahisi kwa mtu yeyote kutangaza takwimu za Taifa au
hata kumkuta akirandaranda maeneo zilipo ofisi za Taifa za takwimu,”
alisema Dk Chuwa.
“Hata
sisi Tanzania, inawezekana kazi ya kusambaza takwimu ikafanywa na Ofisi
ya Taifa ya Takwimu pekee kwa sababu wataalamu tunao wa kutosha,”
alisema.
Kauli
ya Dk Chuwa imetolewa ikiwa ni siku chache baada ya Kiongozi wa Chama
cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe kukosoa takwimu za Aprili na Juni
zilizotolewa na Serikali kwamba hazikuwa sahihi.
Zitto
ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini alisema takwimu za Serikali kuhusu
kasi ya ukuaji wa uchumi katika robo ya pili ya mwaka ni tofauti na
ukokotozi kwa kanuni za kiuchumi.
“Hatujatafuta
takwimu nyingine, hizi ni taarifa zilezile zilizotolewa na BoT (Benki
Kuu ya Tanzania)na NBS lakini ukikokotoa utaona uchumi unasinyaa badala
ya kukua na hali ikiendelea hivi hadi Juni mwakani kutakuwa hakuna
uchumi mwakani,” alikaririwa Zitto.
Katika
kipindi hicho maalumu cha miaka miwili ya Rais John Magufuli, Kamishna
wa Mapato ya Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Elijah
Mwandumbya alisema katika mwaka wa fedha 2016/17, Serikali imesajili
biashara mpya 289,000.
Alisema
jumla ya biashara 20,000 zilifungwa kutokana na kutoendana na kasi ya
Serikali ya Awamu ya Tano ya kulipa kodi stahiki na si kutokana na
mazingira magumu ya biashara kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
“Tulisajili
biashara nyingi 2016/17, hii ni kutokana na jitihada ya Serikali katika
kuhakikisha inaboresha mazingira ya uwekezaji nchini,” alisema
Mwandubya.
Alisema
katika jitihada za kuendelea kuwavutia wawekezaji wengi zaidi, TRA
tangu Novemba Mosi ilianzisha utaratibu wa msamaha wa kodi kwa miezi
mitatu kwa biashara mpya.
Alisema
jitihada hizo zinalenga kuongeza idadi ya walipa kodi ambao kwa sasa ni
milioni 2.5 kati ya vijana 21 milioni wenye nguvu za kufanya kazi, kwa
mujibu wa NBS
SHARE









No comments:
Post a Comment