
Bw. Jeremiah Ragita
aliyejifanya kuwa Wakili akitokea Kampuni ya Sheria ya Faithful Attorney
Advocates kwa mujibu wa Naibu Msajili, Mahakama ya Ardhi, Mhe. Frank
Mahimbali anasema Wakili huyo feki alikamatwa mapema Novemba 08 katika
Mahakama hiyo akimsimamia Mleta maombi Nunu Mhusin Mkwata.
………………………………………………..
Mhe. Mahimbali anasema kuwa
upande wa pili ambao unasimamiwa na Wakili Maros Gabriel kutoka Kampuni
ya Sheria ya ‘Common Law Chambers’ ulimtilia shaka Bw. Jeremiah Ragita
kama kweli ni Wakili ndipo alipofanya upekuzi kwenye Ofisi ya TLS na
kuambiwa kuwa hawana jina hilo.
Hata hivyo Mhe. Mahimbali
alienda mbali na kumuandikia barua Msajili wa Mahakama Kuu (RHC) na
kujibiwa kuwa hakuna Wakili aliyesajiliwa kwa jina hilo.
Kwa mujibu wa Naibu Msajili
kesi hiyo ilipoitwa mbele ya Mhe. Jaji Crencesia Makuru, Wakili Maros
alimueleza Mhe. Jaji kuwa mwenzake wa upande wa pili sio Wakili na kisha
akatoa vielelezo kutoka katika Ofisi ya Msajili Mahakama Kuu na Ofisi
ya TLS ndipo Bw. Ragita akakiri kuwa yeye si Wakili.
Hata hivyo Bw. Ragita
alikamatwa na kupelekwa Polisi Kituo cha Kati (Central Police) jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya hatua stahiki za kisheria.
Mahakama inapinga vikali
vitendo vya ulaghai (Mawakili feki, vishoka) vinavyofanywa na baadhi ya
Wananchi kwa lengo la kujipatia kipato.
(Imetolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Mahakama)
SHARE








No comments:
Post a Comment