
Zikiwa zimebaki siku chache kabla
ya kampuni ya Multichoice Tanzania (DStv) kuanza ofa yake kabambe ya
msimu wa sikukuu, imesema inaanza kuwatunuku wateja wake kwa kuwapa
chaneli za SuperSport bure kwa siku 7 kwa wateja watakaolipia huduma za
DStv kabla ya kukatika
Kwa wateja wa kifurushi cha DStv Compact na DStv Compact Plus watakaofanya malipo ya kifurushi kabla ya kukatika watapata chaneli zote za SuperSport zinazopatikana katika kifurushi cha DStv Premium kwa kipindi cha muda wa siku saba (7) mfululizo bureeee!!!
Kwa wateja watumiaji wa kifurushi DStv Bomba na DStv Family wao watapata chanel zote za
SuperSport zinazopatikana kwenye Kifurushi DStv Compact
na hivyo kuweza kushuhudia mechi zote za Ligi ya Uingereza (PL) na
mashindano mengine makubwa kwa siku saba (7) mfululizo bureee!!!!
Akizungumzia zawadi hii Meneja wa
Wateja wa Multichoice Tanzania Hilda Nakajumo amesema hii itaendelea
kwa muda na ni chombeza tuu kwani baada ya muda mfupi itaanza ofa maalum
ya msimu wa sikukuu. “Mara zote sisi DStv huwa tunawatunuku wateja
wetu, na sasa tumeamua kuwatuza wale wote watakaolipia akaunti zao kabla
hazijakatika kwa kuwapa chaneli za michezo za vifurushi vya juu”
alisema.
“Kuwathamini na kuwasikiliza
wateja wetu umekuwa ni utamaduni wetu endelevu. Na tutaendelea kufanya
hivyo ikiwemo kurekebisha bei zetu, kutoa tuzo na ofa mbalimbali na la
msingi zaidi kuhakikisha kuwa muda wote tunawapa wateja wetu huduma bora
kabisa” alisisitiza Hilda na kuwataka Watanzania wote kukaa mkao wa
kula kwani kuanzia Septemba 15, DStv itazindua ofa yake maalum ya
sikukuu itakayokuwa gumzo hapa nchini.
SHARE








No comments:
Post a Comment