Mkuu wa Kitengo cha Biashara
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa – NIDA Ndugu Thomas William pamoja na
Ndugu Innecent Baraza Meneja Usimamizi wa Majengo (Kushoto) wakifuatilia
kwa karibu Uingizwaji wa taarifa za waombaji wa Vitambulisho vya Taifa
wakati wa Zoezi la Usajili na Utambuzi linaloendelea Mkoa wa Singida.

Wanachi katika Halmashauri ya
Manispaa ya Singida, wakifanyiwa usajili wa Maombi ya Vitambulisho vya
Taifa katika zoezi la Usajili wa Mkupuo (Mass Registration) linaloendela
hivi sasa Mkoani humo.

Baadhi ya Wananchi katika kata ya
Kindai Halmashauri ya Manispaa Singida wakiwa kwenye foleni kuelekea
kwenye chumba cha uchukuaji alama za kibaiolojia, picha na saini ya
kielektroniki.

…………………………………………………………………..
Usajili Vitambulisho vya Taifa
mkoani Singida umezidi kushika kasi wananchi wakifika kwa wingi kupata
huduma ya Usajili unaohusisha uchukuaji wa alama za Kibiolojia, picha
na Saini ya Kielektroniki.
Kwa kushirikiana kwa karibu na
Maafisa Usajili, Watendaji wa Kata na Serikali za Mtaa, watumishi wa
Mamlaka wamekuwa wafakifanya jitihada kubwa za kuhakikisha Wananchi
wanatambua umuhimu wa kuwa na Vitambulisho vya Taifa pamoja na Matumizi
yake Msingi na kushiriki kikamilifu kujisajili.
Pamoja na misururu mirefu
wananchi hao wameonyesha kutokata tamaa kwa foleni ndefu badala yake
wamekuwa wakihamasishana kushiriki ili kila mmoja kupata haki yake
msingi kusajiliwa.
Mkoa wa Singida ni miongoni mwa
mikoa 12 ya Tanzania ambayo zoezi hilo linaendelea kwa sasa ukiwemo mkoa
wa Mbeya, Njombe, Songwe, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza,
Shinyanga, Simiyu, Geita na Iringa.
SHARE
No comments:
Post a Comment