TRA

TRA

Wednesday, December 6, 2017

KALIDUSHI MWENYEKITI MPYA WA CCM MKOA WA GEITA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Wajumbe wakiwa wamembeba mshindi wa kiti cha uenyekiti Mkoani Geita,Alhaji Said Maneno Kalidushi baada ya kuibuka mshindi kwa kura 358.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,MhandisI Robert Luhumbi akizungumza na wajumbe wa  kabla ya kufanyika kwa uchaguzi .

Wananchama wa chama cha mapinduzi (CCM)Mkoani Geita wakifurahia wakati walipokuwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Mwenyekiti  Mstaafu wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Geita Bw. Joseph Kasheku Msukuma akizungumza na wanachama wakati wa uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti ambaye alitakiwa kukalia kiti chake .

Baadhi ya wagombe wakimsikiliza mwenyekiti ambaye amemaliza muda wake wakati wa uchaguzi.

Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ambayo ilikuwa ikisimamiwa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoani Geita,ambaye amemaliza muda wake wakiwaaga wajumbe hili kupisha nafasi mbali mbali ziweze kugombewa.

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi,Bw Hamis Kigwangala akisoma kanuni ambazo zimo kwenye katiba ya chama hicho kabla ya uchaguzi kufanyika.


Wagombea ngazi ya uenyekiti wakiwa wameshikilia namba ambazo zinawasaidia wapiga kula kuwachagua.

Wajumbe wakipiga kura wakati wa zoezi la uchaguzi.

Mwenyekiti  Mstaafu wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Geita Bw. Joseph Kasheku Msukuma  akizungumza na waandishi wa habari.

Mwenyekiti mpya wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Geita Alhaji  Said Maneno Kalidushi  akitoa hotuba yake ya kwanza kuwashukuru wapiga kura mara baada ya kushinda uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Omega  mjini Geita  jana  akiwashinda wapinzani wake wawili   
John Luhemeja na Saimon Mayengo.
(PICHA NA CONSOLATA EVARSIT)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger