Kaimu
Mkurugenzi wa BoT, Tawi la Mtwara, Bi. Leticia Rweyemamu, akitoa hotuba
ya kufunga semina ya sikju tano ya waandishi wa habari za Uchumi,
Biashara na Fedha, kwenye makao makuu ya tawi hilo Mkoani Mtwara leo
Ijumaa Februari 9, 2018.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mtwara
SEMINA
ya siku tano ya waandishi wa Habari za Uchumi, Biashara na Fedha
iliyoandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania, Idara ya Uhussiano na Itifaki,
imemalizika leo Februari 5, 2018 mkoani Mtwara.
Katika
simian hiyo iliyofunguliwa mwanzoni mwa wiki na Naibu Gavana wa Benki
Kuu anayeshughulikia Utawala na Udhibiti wa Ndani (AIC), Bw. Julian
Raphael Banzi, waandishi hao wamejifunza mambo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na mabadiliko ya mfumo mpya wa kuandaa Sera ya Fedha, (Financial
Monetary Policy), mapitio ya maendeleo ya uchumi nchini, kikanda na
dunia, mifuko ya dhamana kwa wajasiriamali na dhamana za serikali.
Mambo
mengine ambayo waandishi hao kutoka vyombo mbalimbali vikiwemo, Redio,
Luninga, Magazeti na Blogs ni kanuni mpya za usimamizi wa bureaux de
change, usimamizi wa mabenki na taasisi za fedha na dhamana kwa mikopo
ya nyumba (Mortgage Finance).
Waandishi
hao pia wamepata wasaa wa kujifunza nafasi ya matawi ya BoT katika
utekelezaji wa majukumu ya benki hiyo, fidia za interoperability katika
kukuza huduma rasmi za fedha ili kujua kuna usalama gani wa fedha za
wateja wanaotumia mifumo ya kufanya miamala ya kampuni za simu.
Lakini
pia wamejifunza kuhusu nafasi ya dodi ya ya amana katika ufilisi na kwa
nini ulipaji fidia kwa wateja wa benki zilizofilisiwa unachukua muda
mrefu, mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa Sera ya Fedha Safi
(Clean Money Policy), mafanikio na changamoto za dawati la kutatua
malalamiko ya wateja wa benki na taasisi za fedha.
Aidha
waandishi hao pia walipata fursa ya kutembelea miradi ya kiuchumi
inayotekelezwa na serikali na taasisi binafsi ya uchimbaji na uc
hakataji wa gesi, huko Mnazi-Bay na Madimba.
Akifunga
semina hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa BoT tawi la BoT, Mkoani Mtwara, Bi.
Leticia Rweyemamu, amewataka waandishi hao kutumia elimu waliyoipata ili
kuhabarisha umma kwa usahihi kuhusu kazi za Benki Kuu, na kutumia faida
waliyopata ya kukutana na wataalamu mbalimbali wa BoT ili wawatumie
kupata ufafanuzi wa habari mbalimbali za kiuchumi ili kuandaa habari
timilifu.
“Nimejifunza
kutoka kwenu kwamba ubora wa habari unategemea idadi ya watoa taarifa
katika habari hiyo na ninatoa rai kuwa watumieni wataalamu hao ipasavyo
ili kuzifanya taarifa zenu kwa wananchi ziwe bora zaidi.” Alisema Bi.
Rweyemamu
Aitoa
wito kwa waandishi hao kutumia utaalamu kuelimisha umma kutumia huduma
rasmi za kibenki ili kutunza fedha na kufanya miamala kwani ni muhimu
kwa sababu licha ya kuhakikisha usalama wa fedha za mtyumiaji wa huduma
hizo kuna uwezekano mkubwa wa kujikinga na upotevu wa fedha unaoweza
kutokea kwa sababu mbalimbalin ikiwemo wizi.
“Pia
toeni uchambuzi wa kina kuhusu taarifa za fedha, (Financial Statements),
za mabenki na taasisi za fedha ili kuwawezesha wananchi waliokuwa na
amana au wangependa kuwekeza amana zao kuwa na taarifa sahihi kuhusu
hali ya taasisi hizo ili kufanya maamuzi sahihi.
“Haitoshi
kuandika kuwa benki fulani imepata faida kiasi Fulani au hasara kiasi
Fulani tu, ni vema wananchi wakapata taarifa mbalimbali zinazohusu
ukwasi wa taasisi husimka, ikiwemo mali, madeni pamoja na mipango
mbalimbali ya taasisi hizo za kifedha.” Alifafanua.
Bi.
Rweyemamu, amewahamasisha waandishi hao kutumia nafasi ya BoT
kuhabarisha namna inavyoandaa na kutekeleza sera ya fedha ili
kuhabarisha umma mwenendo wa uchumi na sekta ya fedha nchini ili
hatimaye wafanye maamuzi sahihi ya kuhusu uwekezaji hapa nchini.
Alivitaka
vyombo vya habari kutumia nafasi kubwa katika kutoa taarifa
zinazochangia maendeleo ya uchumi wa viwanda na kupunguza fursa kubwa
inayotolewa kwa taarifa za kuburudisha tu, kwani kwa kufanya hivyo
vyombo vya bhabari vitaisaidia serikali kuelezea mipango yake ya
kueldekea uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.
“Kama
alivyoeleza Naibu Gavana wakati akifungua semina hii, Benki Kuu
inatambua mchango wa vyombo vya ahabari vyote ikiwemo redio,
televisheni, magazeti na mitandao ya kijamii katika kutangaza habari za
benki hiyo kwa manufaa ya umma.” Kwa upande wake, Kaimu Meneja Uhusiano
na Itifaki wa BoT, Bi. Vicky Msina alisema BoT itaendelea kutoa mafunzo
kwa waandishi wa habari kwani kwa kufanya hivyo kunajenga uwezo wa
waandishi kufanya uchambuzi wa taarifa mbalimbali na kuziandika kwa
usahihi.
“Nimefarijika sana kuwa pamekuwepo na uelewa mkubwa wa waandishi hawa kuhusu utekelezaji na majukumu ya Benki Kuu.” Alisema
Kaimu Meneja wa Idara ya Uhusiano na Itifaki, BoT, Bi. Vicky Msina, akizungumza wakati wa hafla ya ufungaji wa semina hiyo.
Dkt.
Suleiman Missango, Meneja Msaidizi-Idara ya Utafiti, Kurugenzi ya Sera
za Uchumi na Utafiti, BoT, akiwasilisha mada kuhusu Government
securities (Government Date Securities) , mwishoni mwa semina hiyo leo
Februari 9, 2018.
Dkt.
Suleiman Missango, Meneja Msaidizi-Idara ya Utafiti, Kurugenzi ya Sera
za Uchumi na Utafiti, BoT, akiwasilisha mada kuhusu Government
securities (Government Date Securities) , mwishoni mwa semina hiyo leo
Februari 9, 2018.
Meneja
Msaidizi, Dawati la Kutatua Malalamiko ya wateja wa mabenki na taasisi
za fedha, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT) Bw.Ganga Ben Mlipano,
akitambulishwa kwa wana semina kabla ya kuwasilisha mada ya mafanikio na
changamoto za dawati hilo.
Meneja
Msaidizi, Dawati la Kutatua Malalamiko ya wateja wa mabenki na taasisi
za fedha, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT) Bw.Ganga Ben Mlipano,
akiwasilisha mada kuhusu mafanikio na changamoto za dawati la kutatua
malalamiko ya wateja wa benki na taasisi za fedha.
Bw. Ganga akibadilishana maewazo na Bi.Vicky Msina, kabla ya kuwasilisha mada yake.
Mgeni
rasmi, B. Leticia Rweyemamu, (kulia), akiongozana na Bibi.Leah Mzundu,
Meneja Idara ya Uendeshaji Tawila BoT Mtwara, wakati akiwasili ukumbini
kufunga semina.
Kutoka kushoto, Bi. Vicky Msina, Bi. Leticia Rweyemamu na Dkt. Suleiman Missango.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji na wana semina mwishonin mwa semina hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment