Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) mkoa wa
Dar es Salaam Macdonald Maganga akitoa uamuzi wa wao kuwaweka kampuni ya
udalali ya Yono Auction kwa ajili ya kwenda kukamata wadaiwa sugu wote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
udalali ya Yono Auction Mart, Scholastica Kevela akitoa tamko la siku
14 kwa wadaiwa sugu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO),
kulipa madeni yao kabla ya chukuliwa hatua za kisheria ikiwamo mali zao
kupigwa mnada kufidia deni.
Meneja wa SIDO mkoa wa Dar es
Salaam Macdonald Maganga akiongoza wafanyakazi na viongozi wa Yono
kupita mlango kwa mlango wakati wakizundua kampeni ya kudai madeni “LIPA
DENI LAKO SIDO, KUWA MZALENDO’.
Wakiingia katika moja ya ofisi za mdaiwa wa SIDO.
Nae Mwenyekiti wa Kuatamia mawazo
ya wabunifu, Joseph Mlay ameiunga mkono SIDO kwa hatua waliyochukua ya
kuingia mlango kwa mlango katika kudai madeni yao.
Na Cathbert Kajuna – Kajunason/MMG.
Shirika la Kuhudumia Viwanda
Vidogo (SIDO), mkoa wa Dar es Salaam imetangaza vita kwa wale wadaiwa
sugu kulipa madeni yao kabla ya chukuliwa hatua za kisheria ikiwamo mali
zao kupigwa mnada.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar
es Salaam, Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), mkoa
wa Dar es Salaam Macdonald Maganga wakati akizindua kampeni ya kukusanya
madeni kwa wateja wao.
“Leo tunazindua kampeni ya
kukusanya madeni kwa wadaiwa sugu wote wa SIDO hatutakuwa na huruma juu
ya hili maana hawa ndiyo wanarudisha maendeleo ya shirika nyuma, kuna
waliokopa, walipanga kama haujalipa deni lako ujue tunakupa siku 14 tu
baada ya hapo sheria itachukua mkondo wake,” amesema Mkurugenzi Maganga.
Meneja Macdonald Maganga amesema
wadaiwa ni wale waliopewa maeneo maalumu ya viwanda kwa ajili ya
kufanyia kazi zao na waliopatiwa huduma ya fedha kwa mkopo na kushindwa
kurejesha kwa wakati.
“Kuna ambao wamekaa miaka mingi
au miezi mingi bila kurejesha fedha kwetu kama shirika inatuathiri kwa
sababu hatuwezi kuwahudumia wengine,” amesema Maganga.
Maganga amesema wanadai jumla ya sh. milioni 350 kutoka kwa wadaiwa zaidi ya 77.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, Scholastica Kevela
amewashukuru SIDO kwa kuweza kuwapa kazi hiyo ya kuwakusanyia madeni na
kuongeza kuwa hawata muonea huruma mdaiwa yeyote.
“Yono Auction Mart tunatoa siku
14 kwa wadaiwa sugu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO),
kulipa madeni yao kabla ya chukuliwa hatua za kisheria ikiwamo mali zao
kupigwa mnada kufidia deni,”. amesema Mama Kevela.
“Kwa wadaiwa wote wa SIDO,
wanaoishi kwenye viwanda na nyumba za SIDO bila kulipa pango,
waliochukua mikopo na hawataki kurejesha kwa sababu wanazozijua wao,
mkono wa Yono uko kazini ni vyema wakachukua hatua wakalipa ili
kuondosha usumbufu,” amesema Kevela.
Mdaiwa Masoud amedai hawafanyi makusudi kutolipa madeni ni
kutokana na kodi kupanda kila mwaka huku hali ya biashara ikiwa mbaya.
“Ukizingitia soko la ushidani na hali ya bidhaa unashindwa kuuza kwa wakati kwa hiyo tunalipa lakini hatulipi kwa wakati,” amesema.
“Ukizingitia soko la ushidani na hali ya bidhaa unashindwa kuuza kwa wakati kwa hiyo tunalipa lakini hatulipi kwa wakati,” amesema.
Amedai wamepangishwa kwa zaidi ya miaka 40 wakifanya shughuli
zao na kama wangekuwa hawalipi kwa kipindi chote wangefukuzwa hivyo
ameiomba serikali kutodhani kuwa wanapuuza kulipa madeni.
SHARE
No comments:
Post a Comment