Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango, akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara
ya Habari-Bunge mjini Dodoma (hawapo pichani) kuhusu hatua ya Serikali
ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa
Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018.
Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Bajeti, Bw. Emmanuel Tutuba na Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susan Mkapa (Picha-Wizara
ya Fedha na Mipango)
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango, akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara
ya Habari-Bunge mjini Dodoma (hawapo pichani) kuhusu hatua ya Serikali
ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa
Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018.
Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Bajeti, Bw. Emmanuel Tutuba na Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susan Mkapa, kulia ni
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa Wizara hiyo Bw. Richard Mkumbo
(Picha-Wizara ya Fedha na Mipango)
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango, akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara
ya Habari-Bunge mjini Dodoma (Hawapo Pichani)kuhusu hatua ya Serikali
ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa
Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018.
Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Bajeti, Bw. Emmanuel Tutuba na Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susan Mkapa, kulia ni
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa Wizara hiyo, Bw. Richard Mkumbo
(Picha-Wizara ya Fedha na Mipango)
…………………………………………………………………………….
TAARIFA YA WAZIRI WA FEDHA KUHUSU MALIMBIKIZO YA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI
Ndugu Wawakilishi wa vyombo vya
habari, nimewaiteni leo hii ili niwape taarifa fupi kuhusu malipo ya
madai ya malimbikizo ya mishahara kwa Watumimishi wa umma waliokuwa na
madai ili muweze kuufikishia umma wa Watanzania.
Serikali kupitia mfumo wa taarifa
za kiutumishi na mishahara (Human Capital Management Information System
– HCMIS) kufikia tarehe 01 Julai 2017 ilikuwa na madai ya malimbikizo
ya mishahara yenye jumla ya shilingi 127,605,128,872.81 kwa watumishi
82,111 Wakiwemo walimu 53,925 waliokuwa wanadai shilingi
53,940,514,677.23 sawa na asilimia 42.27 ya madai yote, na wasiokuwa
walimu 28,186 waliokuwa wanadai jumla ya shilingi 73,664,614,195.58 sawa
na asilimia 57.73 ya madai yote. Madai haya yalikuwa ya muda mrefu
mengine yakiwa ya kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2017
Madai haya yalijumuisha mishahara
isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na nyongeza za
mishahara zilizotokana na kupandishwa vyeo na kuchelewa kurekebishiwa
mishahara.
MATOKEO YA UHAKIKI WA MADAI YA SHILINGI BILIONI 127,605,128,872.81 KWA WATUMISHI 82,111
- Madai ya watumishi 27,389 kati 82,111 yenye jumla ya shilingi 43,393,976,807.23 ikiwa ni asilimia 34 ya madai yote ya shilingi bilioni 127,605,128,872.81 yaliyohakikiwa yameonekana ni sahihi na yanastahili kulipwa bila marekebisho.
- Madai yanayostahili kulipwa yanajumuisha shilingi bilioni 16.25 kwa walimu 15,919 na shilingi bilioni 27.15 kwa watumishi wasiokuwa walimu 11,470
- Madai yote yaliyoonekana kuwa sahihi ya shilingi bilioni 43.39 yatalipwa pamoja na mshahara wa mwezi Februari 2018 kwa mkupuo mmoja. Malipo ya Madai haya ambayo mengine yana zaidi ya miaka kumi majina ya walipwaji wote yatatangazwa kwenye magazeti kuanzia kesho tarehe 10 Februari, 2018.
Kwa matokeo hayo ya uhakiki,
mazoezi yaliyofanyika likiwemo zoezi la kuwaondoa kwenye Mfumo wa
malipo ya mshahara (“payroll”) watumishi hewa, vyeti feki na wasio kuwa
na sifa na uhakiki wa madai ya malimbikizo ya mishahara uliofanyika
limeweza kuokoa jumla ya shilingi bilioni 84.22 ambazo ni sawa na
asilimia 66 ya madai yote ya malimbikizo ya awali ya shilingi bilioni
127.61 yaliyokuwa kwenye mfumo ambazo bila zoezi la uhakiki kufanyika
zingelipwa wakati zilikuwa hazistahili kulipwa.
Serikali itaendelea kulipa madai
ya watumishi kadiri yanavyojitokeza ili kuondokana na malimbikizo ya
aina hii ambayo yanaweza kuisababishia Serikali hasara kwa kulipa madai
yasiyostahili.
SHARE
No comments:
Post a Comment