Viongozi mbalimbali wa Chadema wakiongozwa Katibu Mkuu wa Chadema Dr Vicent Mashinji, Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Edward Lowasa, Waziri Mkuu Msaatafu Sumaye na Meya wa Jiji la Arusha Mjini Kalisti Lazaro wakiwa mahakamani .
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe Naibu Katibu Mkuu Chadema John Mnyika ,pamoja na Viongozi mbalimbali wakiwa mahakamani leo.
View attachment 476314
Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiwa nje ya Mahakama Kuu ya Arusha baada ya Mawakili wa Jamuhuri kuomba kuwasilisha hoja ambayo wamekwenda kuiandaa kwa dakika 15 na Jopo la Mawakili wa Utetezi likiwakilishwa na Wakili Msomi Peter Kibatala,wameomba dakika 60 ili kujiandaa kujibu hoja hiyo ya mawakili wa Jamuhuri..
Mahakama Kuu Arusha inatarajia kutoa maamuzi ya dhamana na Godbless Lema saa saba na nusu mchana. Mawakili wamepewa muda kujibu hoja zilizotolewa.
Viongozi mbalimbali wa Chadema wanaanza kuingia mahakamani kusubiri uamuzi wa Jaji Magimbi kuhusu dhamana ya Mbunge Godbless Jonathan Lema.
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Mjini baada ya kupitia hoja za mawakili pande zote imemwachia kwa dhamana Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema. Ameachiwa kwa dhamana ya masharti ya wadhamini wawili na kusaini bondi ya shilingi milioni moja.
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema akiwa kwenye gari baada ya kuachiwa kwa dhamana leo.
SHARE
No comments:
Post a Comment