Mwanachama
na kijana tajiri barani Afrika kwa sasa Mohammed Dewji anayetaka
kununua hisa Simba, amesikitishwa na uongozi wa klabu hiyo kwa kuingia
mkataba wa udhamini na kampuni ya SportPesa bila kumshirikisha.Na habari
ambazo hazijathibitishwa na upande wowote, zinasema Mo Dewji, Mbunge wa
zamani wa Singida Mjini ameuandikia barua uongozi wa klabu hiyo chini
ya Rais wake, Evans Aveva kudai alipwe fedha zake, Sh Bilioni 1.4
alizokuwa anaikopesha Simba kwa kulipa mishahara ya wachezaji na benchi
la Ufundi, Sh Milioni 80 kila mwezi.Imedaiwa Mo Dewji alikuwa anatoa
fedha hizo kwa makubaliano zitalipwa wakati mpango wake wa kununua hisa
za klabu utakapokamilika. Mo alikubaliana na uongozi wa Simba kununua
asilimia 51 ya hisa kwa Sh. Bilioni 20 mara baada ya mchakato wa
mabadiliko ya Katiba utakapokamilika.Lakini zoezi hilo linaelekea
kuingia doa baada ya Mo Dewji kuandika katika ukurasa wake wa Twitter
akilalamikia uongozi wa klabu kuingia mkataba na SportPesa bila
kumshirikisha.
Na upande
mwingine, uongozi wa Simba na umemeguka baada ya Mjumbe wa kuteuliwa wa
Kamati ya Utendaji wa usajiri, Zacharia Hans Poppe ameandika barua ya
kujiuzulu, naye pia akilalamikia kutoshirikishwa katika mkataba wa
SportPesa.
Hans
Poppe aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Kamati za Usajili na mradi wa ujenzi
wa Uwanja wa Bunju Complex, amethabitisha kujiuzulu kwake, lakini
hakutaka kuzama ndani zaidi juu ya sakata hilo.
Ijumaa
SportPesa Tanzania ilitangza rasmi udhamini wake wa miaka mitano kwa
klabu ya Simba ya Dar es Salaam, wenye thamani ya Sh. Bilioni 4.96.
Mkurugezi
wa Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema kwamba wameingia mkataba
huko kwa dhumuni la kuendeleza soka nchini na kuisaidia klabu ya Simba
kufikia malengo yake.
Akifafanua,
Tarimba ambaye ni Mwenyekiti wa zamani wa mahasimu wa Simba, Yanga
alisema kwamba, katika mkataba wao kwa mwaka wa kwanza wadhamini hao
watatoa Sh. Milioni 888 na miaka itakayofuata wataongeza asilimia 5 na
miaka miwili ya mwisho watatoa Sh. Bilioni 1 na kwamba fedha hizo
zitatolewa kwa awamu nne kwa mwaka.
Tarimba alisema kwamba Simba watapaswa kuyathibitisha matumizi ya fedha hizo kwamba yalifanyika kwa maendeleo ya soka.
Alisema
licha ya mkataba huo, pia kutakuwa na motisha klabu hiyo ikishinda
mataji, mfano kwa ubingwa wa Ligi Kuu watapewa zawadi ya Sh. Milioni
100.
“Pia
ikishinda michuano kama (Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati) Kombe la
Kagame pia watapewa zawadi na wakifanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa
Afrika watapata zawadi ya Milioni. 250,”alisema Tarimba.
SHARE
No comments:
Post a Comment