Mbunge
wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika kivuko ambacho si salama
kuelekea upande wa pili alipotembelea kijiji cha tambani ambao wamekosa
mawasiliano leo.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mbunge
wa Mkuranga, Abdallah Ulega amewatembelea wananchi wa Kijiji Tambani
ambao hawana mawasiliano ya kuvuka kwenda kutokana na daraja kuchukuliwa
na maji. Akizungumza na wananchi cha Tambani, Ulega amesema kuwa mvua hizo zimeleta athari hivyo unahitajika ufumbuzi wa haraka.
Amesema
usafiri wa mitumbwi si salama katika kutoa huduma ya usafiri kwa
wananchi wa kijiji cha tambani na maeneo mengine. Kutokana na wananchi
hao kukosa mawasiliano Mbunge huyo ametoa sh.milioni moja pamoja na
mifuko ya saruji 100 ili kuweza kutengeneza daraja hilo.
Wananchi
wa kijiji hicho kwa kila kaya wamekubalina kutoa sh.10,000 ambazo
zitafanya kazi katika ujenzi wa daraja hilo pamoja na nguvu zao
zitatumika. Diwani wa Tambani, Ally Mtamilwa amsema kuwa ujio wa Mbunge
wa jimbo la Mkuranga ameeta matumaini kwa wananchi na kuahidi nae kutoa
mifuko 20 ya saruji.
Mbunge
wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika kivuko ambacho si salama
kuelekea upande wa pili alipotembelea kijiji cha tambani ambao wamekosa
mawasiliano leo.
Wananchi
wakiwa katika kivuko ambacho si salama kwa safari baada daraja la
kijiji hicho kusombwa na maji leo kufuatia mvua iliokuwa ikinyesha
maeneo mbalimbali nchini.
Wananchi
wakisubiri kivuko ambacho si salama na kuwagharimu kulipa sh.500 kwa
kila safari wanayoifanya kwenda katika vijiji vingine kupata mahitaji
.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii )
Mbunge
wa Mkuranga , Abdallah Ulega akizungumza na wananchiwa wa kijiji cha
Tambani ambao wamekosa mawasiliano kutokana na daraja kuchukuliwa na
maji leo.
Diwani wa Tambani , Ally Mtamilwa akizungumza na wananchi wake wakati wa ziara ya mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega.
Mbunge
wa Mkuranga , Abdallah Ulega akikabidhi msaada wa sh.milioni moja kwa
ajili ya ujenzi wa daraja lilichukuwa na maji katika kijiji cha Tambani.
SHARE
No comments:
Post a Comment