FMh:Mwigulu
Nchemba akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI
Mh:Simbachawene wakiwasili kwenye eneo la machinjio ya Vingunguti
kwaajili ya kutoa majawabu kutokana na kero mbalimbali zinazowakabili
wadau wa machinjio hayo.Mwigulu
Nchemba akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh:Simbachawene
wakikagua eneo la machinjio ya Vingunguti kabla ya kuzungumza na wadau
wa eneo hilo pamoja na uongozi wake.
Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na Mh:Simbachawene wakielekea kuzungumza na wananchi wanaotumia Machinjio ya vingunguti.Mawaziri
kutoka kulia ni Naibu waziri wa Afya Mh:Kigwangallah,Wa pili kutoka
kulia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Mh:Bonah,Watatu kutoka kulia ni
Mh:Simbachawene na wa mwisho kushoto ni Mh:Mwigulu Nchemba wakijadiliana
jambo.Mkutano ukiendelea wa kutoa majawabu kuhusu changamoto za Machinjio ya Vingunguti.Mh:Simbachawene
akiwaagiza watumishi wote wa Machinjio ya Vingunguti kuripoti ofisini
kwake Jumanne wakiwa na mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.Mh:Mwigulu
Nchemba akizungumza na Wananchi(Wadau) wa machinjio ya Vingunguti
kuhusu hatua za kinidhamu alizozichukua kwa Mkuu wa mnada wa pugu
inakotoka mifugo kabla ya kufika Machinjio ya Vingunguti kwa upotevu wa
mamilioni ya shilingi ya kodi za serikali.Mawaziri wakiagana na wananchi mara baada ya mkutano wa kutatua kero zao za Machinjio kumalizika.Furaha
ya Wananchi mara baada ya kutatuliwa kero zao kwa hatua za
awali,wananchi wanasukuma gari la Mh:Mwigulu Nchemba kama ishara ya
kukubali hatua alizochukua.
Ile kauli ya HAPA KAZI TU imeendelea
kutumika vizuri kwa mawaziri wa Mh:Rais J.Magufuli mara baada ya tukio
la mawaziri watatu kufika eneo la Machinjio ya Vingunguti kwaajili ya
kutatua kero zinazowakabili wananchi wanaotumia eneo hilo kwa shughuli
za kuchinja mifugo.
Awali,Mh.Mwigulu Nchemba alifanya ziara
ya kushitukiza usiku wa tar 01/01/2016 katika machinjio hayo na kukutana
na madudu ya kutafunwa kwa fedha za ushuru unaokusanywa kwenye
mifugo,lakini pia hali ya mazingira ya kutoridhisha ya Machinjio hayo.
Hii leo mapema majira ya saa
3:asubuhi,Mwigulu Nchemba anarejea tena kwenye machinjio hayo akiwa
ameongozana na mawaziri wawili ambao ni Mh:Simbachawene(TAMISEMI) na
Mh:Kigwangallah(AFYA) ambao wote wanagushwa na machinjio hayo.
Mara baada ya kusikiliza kero na maoni ya pande zote mbili,Mawaziri hao waliamua kuchua hatua zifuatazo kwa wahusika.
Mwigulu Nchemba ameagiza Mkuu wa mnada
na watumishi waliokuwa zamu tar 24/12/2015 na tar 01/01/2016 watafute
kazi nyingine kuanzia sasa,Vilevile wahakikishe jumatatu wanafika ofisi
ya Katibu Mkuu wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
Pili,Mwigulu Nchemba ameagiza kuanzia
sasa amesitisha ukusanyaji wa ushuru kwenye eneo la mnada wa pugu,badala
ya hapo makusanyo yote yatafanyika eneo la machinjio la Vingunguti kwa
kutumia mashine za kielektroniki za EFD.
Tatu,Mwigulu Nchemba ameagiza
wananchi(wadau) kuanzia leo waanze kutumia eneo lililokuwa limetengwa
kwaajili ya kutunzia nyama,Eneo hilo awali lilisitishwa bila sababu
maalum na umeme ukakatwa.
Mwigulu Nchemba ameagiza umeme urudishwe hii leo na wananchi waanze kutumia eneo hilo.
Wakati huohuo,Waziri wa TAMISEMI
Mh:Simbachawene ameagiza watumishi wote wa machinjio hayo kujitathimini
na kufika Jumanne waripoti ofisini kwake wakiwa na mkurugenzi kwaajili
ya hatua Zaidi.
Simbachawene ameenda mbali Zaidi kwa
kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha fedha
zinazokusanywa kwenye machinjio hayo zinatumika haraka kujenga
miundombinu ya eneo hilo ilikuendana na wingi wa watu wanaotumia
machinjio hayo.
Kwa upande wa Afya,Naibu waziri wa Afya
Mh.Kingwangallah ameagiza daktari wa machinjio hayo Ndg.Juma aache kutoa
huduma eneo hilo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo,Pia upimaji wa
afya kwa wanaotumia machinjio hayo uwe wa bure na Uongozi wa machinjio
utenge ofisi maalu ya kupima watu hao.
SHARE
No comments:
Post a Comment