Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani)
katika Ofisi ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye na Kushoto ni Nahodha
wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Ali Samatta.
Nahodha
wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Ali Samatta
akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu ushindi wa
kuwa mchezaji bora Afrika alioupata hivi karibuni.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Zawadi ya jezi kutoka kwa Nahodha wa Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Ali Samatta.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoja na Nahodha wa
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Ali Samatta.(PICHA NA
RAYMOND MUSHUMBUSI MAELEZO).
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Rais
mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Ali Samatta
kwa kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi
za Ndani Afrika kwa mwaka 2016.
Pongezi
hizo amezitoa leo Jijini Dar es salaam alipokuta na Naodha huyo katika
Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizopo Lumumba Jijini Dar es
salaam.
Dkt.Kikwete
alimpongeza Nahodha huyo (Mbwana Samatta) na kumtaka kuongeza juhudi
zaidi ili aweze kucheza katka Ligi kubwa Barani Ulaya.
“Natamani
siku moja tuwe tunakuangalia Samatta ukifunga magoli katika Ligi kubwa
Barani Ulaya kama vile Ligi kuu ya Uingereza” Alisema Dkt Kikwete.
Kwa
upande wake, Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Nnauye alisema kuwa Wizara imepata faraja kubwa kwa Samatta kuiwakilisha
Tanzania katika tuzo hizo za Kimataifa kwa kuibuka mshindi katika
kinyang’anyiro hicho.
Aidha,
Mbwana Samatta alisema kuwa, anamshukuru Rais mstaafu Mhe. Dkt. Kikwete
kwa kumpa moyo wa kupambana na ameishukuru pia Serikali ya Awamu ya tano
kwa kumuunga mkono katika kupeperusha bendera ya taifa katika soka la
kimataifa.
Samatta
aliibuka kuwa Mchezaji Bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za
ndani ya Afrika baada ya kuwabwaga wenzake wawili kwenye kinyang’anyiro
hicho, akiwemo mchezaji mwenzake wa TP Mazembe,Kipa Robert Kidiaba
pamoja na Mualgeria,Baghdad Boundjah anayeichezea Klabu ya Etoile Du
Sahel ya nchini Algeria.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment