DC,
Makonda (kulia) akipokea mfuko wa saruji kutoka wawakilishi wa Global,
Elvan Stambuli (katikati) na David Mwaipaja (kushoto).
Elvan
Stambuli (katikati) akionesha risiti ya makabidhiano hayo kutoka kwa
Makonda (kulia), anayeshuhudia kushoto ni Ofisa Masoko wa Global, David
Mwaipaja.
Mkuu wa Wilaya, Makonda (kulia), akionekana kutumia nguvu kubeba saruji wakati wa makabidhiano hayo. Mwakilishi wa Osyter Bay Pharmacy, Kefa Kijo (kulia) akimkabidhi saruji Makonda.
Mwakilishi wa Global, Mhariri Mwandamizi, Elvan Stambuli, akihojiwa na wanahabari mara baada ya makabidhiano hayo.
DC, Makonda (kulia) akipokea mfuko wa saruji kutoka wawakilishi wa Global, Elvan Stambuli na David Mwaipaja.
KAMPUNI
ya Global Publishers Ltd inayozalisha magazeti ya Championi, Uwazi,
Amani, Risasi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda, mapema leo imechangia mifuko
100 ya saruji katika ujenzi wa shule za sekondari wilayani Kinondoni,
Dar.
Mifuko hiyo imekabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda,
na mwakilishi mwandamizi wa Global, Elvan Stambuli, katika ofisi yake
iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam.
“Nikiwa
mwakilishi kutoka Global Publishers, ninakabidhi mifuko 100 kwa ajili
ya kuchangia ujenzi wa sekondari kwa Wilaya ya Kinondoni kutokana na
kuguswa na wito wa mkuu wa wilaya hii alioutoa kwa makampuni na taasisi
mbalimbali kusaidia kuongeza shule saba za sekondari wilayani Kinondoni
ili vijana waweze kupata elimu vizuri,’’ alisema Stambuli.
Wakati
huohuo, naye mwakilishi kutoka kampuni ya Ubapa Limited, Wenceslaus
Rwezahula, na mwakilishi wa Oyster Bay Pharmacy, Kefa Kijo, walitoa
mifuko ya saruji kuchangia ujenzi huo.
Hata hivyo mara baada ya makabidhiano hayo, Makonda aliishukuru Kampuni
ya Global Publishers kwa kuchangia mifuko 100 akisema ni mfano wa kuigwa
kwa makampuni mengine, huku akisisitiza kuwa bado taasisi na makampuni
mengine yanayo fursa ya kuendelea kuchangia ujenzi huo.
PICHA/HABARI: DENIS MTIMA/GPL
SHARE
No comments:
Post a Comment