T
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu
Hassan, akizungumza jambo na Mganga Mfawidhi wa Hospitali teule ya Mkoa
wa Geita, Dkt. Adam Sijaona, wakati alipofanya ziara kwenye wadi ya
wagonjwa wa upasuaji ya wanaume, katika Hospitali hiyo iliyojengwa kwa
ufadhili wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM).
PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, GEITA.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwasalimia baadhi ya wananchi wa Mji wa Geita waliokuwepo Hospitalini
hapo leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (kulia) wakati wa ziara yake katika
Hospitali teule ya Mkoa wa Geita, leo Januari 5, 2016. Kulia kwake ni
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mh. Fatma Mwassa pamoja na Mbunge wa Viti Maalum
Geita Mjini, Mh. Vick Kamata.
MAKAMU
wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu, leo Januari
5, 2016 amezindua miradi ya maendeleo katika mkoa wa Geita
iliyofadhiliwa na mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa ushirikiano na
serikali ya Tanzania.
Mradi
mkubwa wa maji wenye thamani ya Tshs 12Billion uliojengwa kwa
ushirikiano kati ya Mgodi na serikali ambao utapunguza tatizo la maji
safi na salama kwa mkoa wa Geita kwa zaidi ya asilimia 35% umezinduliwa,
ambapo kwa mara ya kwanza, wananchi wa Geita wataweza kunywa maji safi
na salama kutoka Ziwa Zictoria.
Tatizo
la maji lilikuwa ni kero kubwa kwa wakazi wa Geita kwa miaka mingi
ambapo kina mama na watoto wa kike wamekuwa ndio wakiathirika wakubwa
kwa kutembea umbali mrefu ili kupata maji safi kwa matumizi ya nyumbani.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, Makamu wa Rais alisema “Serikali ya awamu ya
tano imekusudia kuleta maendeleo ya kasi kwa Wananchi kwa kushirikiana
na wadau mablimbali wa maendeleo kama inavyodhihirika katika mradi huu”
Makamu
wa Rais aliweza pia kutembelea na kuzindua muendelezo wa hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Geita ambayo ilijengwa mwaka 1957. GGM imeweza kutoa
ufadhili wa ukarabati wa majengo hayo kwa thamani ya zaidi ya shilingi
800 Milioni ambapo ukarabati umekwenda sambamba na utoaji wa vifaa adimu
kwa ajili ya vipimo na matibabu ya moyo, meno nk. Hospitali hii teule
inahudumia zaidi ya wagonjwa milioni 1.7 kwa mwezi.
“Ni
kusudio la GGM kuona kuwa jamii inayotuzunguka inakuwa katika hali nzuri
na bora kuliko hapo mwanzo kwa kuwepo kwetu hapa Tanzania. Hii ni
sehemu ya kutimiza dhamira yetu hii na tunaishukuru serikali ya Tanzania
kwa ushirikiano wake thabiti na kwa kuweka mazingira mazuri ya
utendaji” alisema Mkurugenzi Mkuu wa GGM, Terry Mulpeter.
Miradi
mingine aliyoweza kutembelea na kuzindua ni mradi wa ushonaji na
kutarizi ulio chini ya mradi mkubwa wa kuendeleza uchumi kwa Wananchi wa
Geita uitwao Geita Economic Development Program (GEDP) ambao unahusisha
miradi ya kilimo cha Mpunga na Alizeti, Kufyatua Matofali ya
Interlocking blocks na Uchomeleaji utakaoweza kuleta ajira zaidi ya 300
kwa vijana wa mkoa wa Geita.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akipokea taarifa ya Hospitali teule ya Mkoa wa Geita, kutoka kwa Mganga
Mkuu wa Mkoa, Dkt. Joseph Kisala mara baada ya kuisoma. Katikati ni Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Mh. Fatma Mwassa.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akizungumza na wananchi pamoja na wauguzi wa Hospitali teule ya Mkoa wa
Geita.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akipokea moja vifaa tiba vilivyokabidhiwa hospitalini hapo na Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM), Terry Mulpeter, ikiwa ni
sehemu ya mchango wao kwa jamii ya watu wa Geita, leo Januari 5, 2016.
wengine pichani toka kulia ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mh. Suleiman
Jaffo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mh. Fatma Mwassa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Geita, Dkt. Joseph Kisala, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Mganga Mfawidhi wa Hospitali
teule ya Mkoa wa Geita, Dkt. Adam Sijaona.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akikabidhi vifaa hivyo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita, Dkt. Joseph
Kisala, mara baada ya kukabidhiwa na Uongozi wa Kampuni ya Geita Gold
Mining ambao wamekuwa ni wadau wakubwa wa maendeleo ya Mkoa wa Geita.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM), Terry
Mulpeter, tuzo ya maalum ya kutambua Mchango wa Kampuni hiyo, kwa
kujitoa kwake kuisaidia jamii ya watu wa Geita.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimtishwa ndoo ya maji, Bi. Tatu Salum, Mkazi wa kijiji cha Nyankubi
Mkoani Geita, mara baada ya kuuzindua mradi mkubwa wa Maji Mkoani humo
leo. Nyuma yake ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mh. Gerson Lwenge.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyankubi Mkoani Geita, mara baada
ya kuuzindua mradi mkubwa wa Maji Mkoani humo leo.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mh. Gerson Lwenge, akizungumza na wananchi wa
Kijiji cha Nyankubi Mkoani Geita, mara baada ya kuuzindua mradi mkubwa
wa Maji Mkoani humo leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mh. Fatma Mwassa, wakati
wakitoka kwenye uzinduzi wa Mradi wa Maji.
Sehemu ya wanachama wa Ushirika wa Ushonaji wa Nyakayoma wakimsikiliza Makamu wa Rais.
Mwenyekiti
wa Ushirika wa Ushonaji wa Nyakayoma ambao umewawezesha vijana wa Mkoa
wa Geita kujifunza na kujiajiri, Bi. Debora Mashauri akisoma risala ya
ushirika huo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Samia Suluhu Hassan (Kulia).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wanaushirika huo.
Sehemu ya Mashine za ushonaji zilizotolewa na Kampuni ya Geita Gold Mining.
SHARE
No comments:
Post a Comment