Mr
Blue amesema hana tatizo na Diamond Plutnumz licha ya hivi karibuni
kuibuka sintofahamu katika mitandao ya kijamii juu ya nani mmiliki
halali wa jina ‘Simba.
Blue
ambaye anajipanga kuachia wimbo mpya akiwa na Alikiba mwezi huu,
amekiambia kipindi cha The Weekend Chart Show cha Clouds TV kuwa aliamua
kuweka wazi kwa umma juu ya umiliki ya jina hilo kama namna ya
kusherehekea mafanikio baada ya wasanii kadhaa kumuiga.
“Kile
kitu hakikuwa drama au ugomvi na mtu mimi nilifanya kama kujipongeza,
kwa sababu kama wewe ni shabiki yangu na unanifuatilia vizuri kipindi
cha nyuma nilikuwa napost simba na slogan yangu ‘Simba kaamka na njaa
kali’ yaani baada ya kukaa muda mrefu bila ngoma nilivyokuja kutoa
‘Pesa’ nikaandika Simba kaamka na njaa kali,” alisema.
Aliongeza,
“Pia nilitumia jina Simba kutokana kuwa na sauti ya kukwaruza kwenye
muziki wangu. Sasa siku zinavyokwenda nikaona baadhi ya wasanii wengi tu
sio Diamond wengine wapo Mwananyamala huko,Kigogo wanatumia jina la
Simba. Ikanipa moyo kwamba kitu ambacho nimekigundua watu wamekikubali.
“Kwahiyo
nikapost kitu kwa kujipongeza kwa kitu nilichokigundua miaka 2/3 nyuma
leo kila mtu anataka kutumia. Lakini sasa mashabiki wanaichukulia vibaya
kwa sababu ana mashabiki wengi, angechukua mtu ambaye yupo chini yangu
nadhani yasingetokea haya, kwahiyo naomba ieleweke mimi sina ugomvi na
Diamond na sijawahi kuwa na ugomvi na Diamond.”
Chanzo: Bongo5
SHARE
No comments:
Post a Comment